Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha mikutano cha kimataifa cha AICC,Ephraim Mafuru akizungumza katika kikao hicho na waandishi wa habari jijini Arusha leo.
Mwenyekiti wa jukwaa la viongozi wa Taasisi za umma,Sabasaba Moshingi akizungumza kuhusu maandalizi ya mkutano huo jijini Arusha leo.
RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kesho agosti 19 katika mkutano wa wenyeviti wa Taasisi za umma na wakurugenzi watendaji ambao utafanyika katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha leo Mwenyekiti wa jukwaa la viongozi wa Taasisi za umma ,Sabasaba Moshingi amesema kuwa,jumla ya Taasisi 248 zinatarajiwa kushiriki katika mkutano huo vikiwemo vyuo mbalimbali hapa nchini.
Moshingi amesema kuwa,huo utakuwa ni mkutano wa kwanza kufanyika ambapo watakuwepo viongozi mbalimbali akiwemo Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa pamoja na baadhi ya mawaziri.
Aidha amesema kuwa, mkutano huo utakuwa na kauli mbiu ya “uelekeo mpya wa usimamizi na uendeshaji wa Taasisi za umma kwa matumizi chanya katika kukuza uchumi wa Taifa “amesema Moshingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha mikutano cha AICC ,Ephraim Mafuru amesema kuwa,maandalizi ya mkutano huo tayari yamekamilika na mkutano huo unaratibiwa na ofisi ya Msajili wa hazina na mbali na mkutano huo pia kutakuwepo na maonyesho katika viwanja hivyo vya AICC ambapo zaidi ya wageni elfu mbili watakuwepo katika mkutano huo.
Aidha amewataka wakazi wa mkoa wa Arusha kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha na kuwakarimu wageni watakaofika katika mkutano huo ili Arusha iendelee kuwa mfano wa kuigwa.
Kwa upande wa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) ,Justina Mashiba amesema kuwa,mkutano huo ni wa kwanza kufanyika ambapo kamati ya maandalizi wapo tayari na kupitia mkutano huo kutakuwepo na mabadiliko makubwa mpya .
Amesema kuwa,mkutano huo utaanza agosti 19 hadi 21 ambapo mkutano huo unalenga kuleta mabadiliko mbalimbali ya teknolojia kupitia kwa wakuu hao wa Taasisi na wenyeviti kutoka mikoa mbalimbali.
Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amesema kuwa ,mkutano huo una manufaa makubwa sana kwa mkoa wa Arusha na Taifa kwa ujumla kwani Taasisi za umma zina mchango mkubwa sana katika kusimamia fursa mbalimbali.
“Sisi kama mkoa wa Arusha tunaahidi kuwa tayari wakati wote pale tutakapohitajika ili kufikia malengo yaliyopangwa na kufikiwa kwa wakati uliowekwa.’amesema Mongela.
Aidha amewataka wana Arusha kuwa wakarimu kwa wageni watakaokuwa mkoani Arusha huku wakiendeleza sifa yao ya kulinda wageni na kutoa huduma kwa kiwango cha juu.
No comments:
Post a Comment