RAIA WA BURUNDI KUTUMIKIA KIFUNGO MAHAKAMA YAAMURU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 18 August 2023

RAIA WA BURUNDI KUTUMIKIA KIFUNGO MAHAKAMA YAAMURU


Raia 59 wa Burundi wamelazimika kuanza kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela, baada ya kushindwa kulipa faini ya Sh500, 000; iliyokuwa imeamriwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.


Mahakama hiyo iliwahukumu raia hao kulipa faini hiyo au kwenda jela mwaka mmoja baada ya wao kukiri makosa ya kuingia na kuishi nchini kinyume na sheria.


Pia mahakama hiyo imetoa amri kuwa baada ya raia hao kutumikia adhabu hiyo, warudishwe nchini kwao.


Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi, Ushindi Swalo, ambaye amesema: “Washtakiwa wamekiri mashtaka ya kuingia nchini bila kibali maalumu, na kuishi kinyume na sheria...baada ya washitakiwa kukiri makosa yanayowakabili, mahakama inawahukumu kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh500, 000.”


"Ili iwe fundisho kwa wengine Kwa sababu haya makosa yamekithiri, hivyo mnatakiwa kulipa faini ya Sh500, 000 au kwenda jela miezi 12 na pia baada ya kutumikia adhabu hiyo warudishwe nchini kwao," amesema Hakimu Swalo.


Awali Wakili Mkuu Mwandamizi wa Serikali, Godfrey Ngwijo, aliwasomea maelezo ya awali washitakiwa hao ambapo walikiri makosa yanayowakabili.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso