NA PAUL KAYANDA-SHINYANGA
Mkulima wa kijiji cha Lyagiti kata ya Lyabukande halmashauri ya Shinyanga vijijini, Shauri Elias Mbelele amemuomba Waziri wa Kilimo Husen Bashe amtembelee ili aweze kuona kilimo chake cha umwagiliaji na namna kilivyoathirika hatua ambayo serikali inaweza kumsaidia kupiga hatua Zaidi.
Elias amesema jumla ya ekari 40 za mahindi alizolima zimeathirika kutokana na kukosa maji baada ya mabwawa aliyochimba kienyeji kukauka maji na kupelekea kupata hasara.
Amesema hizo ambazo amelima kwa sasa huenda nazo zikateketea kwa kukosa maji na kumsababishia hasala kubwa kwa mana hiyo anamuomba Waziri wa kilimo Husen Bashe amtembelee ajionee mwenyewe jambo ambalo ataunga juhudi za mkulima huyo.
Pamoja na mambo mengine mkulima huyo ameiomba serikali iweze kusaidia kuchimba mabwawa kitaalamu ili alime kilimo chenye tija Zaidi na kutokana na maji mengi yatakayotosheleza kilimo chake cha umwagiliaji ambacho amekuwa akilima mara mbili kwa mwaka na huku zkitegemez kimpatie kipato na familia yake.
No comments:
Post a Comment