Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetangaza kuwepo kwa upepo mkali unaofikia kilomita 40 kwa saa na mawimbi makubwa yanayofikia mita mbili kuanzia leo huku ikiyataja maeneo ambayo yataathirika ambayo ni maeneo ya maziwa makuu ikihusisha Ziwa Nyasa na Ziwa Victoria.
Meneja wa ofisi kuu ya utabiri ya mamlaka hiyo Dkt Mafuru Biseke, ameitaja mikoa ambayo itaathirika na hali hiyo kuwa ni pamoja na Kagera, Mwanza, Simiyu na Mara ingawa katika Ziwa Tanganyika ni mkoa wa Kigoma, Katavi pamoja na Rukwa huku na Ziwa Nyasa ni Songea pamoja na Njombe.
Huku Jiji la Dar es Salaam pamoja na mikoa mingine iliyopo mwambao wa Pwani kama vile ya Tanga, Visiwa vya Unguja na Mafia ikiwa na uwezekano wa kukumbwa na hali hiyo.
"Tunaomba wananchi kuchukua tahadhari kwani upepo huu una madhara kwa kuwa si upepo wa kawaida na utadumu kwa siku tano," amesema Dk Mafuru.
Kuhusu kuanza kwa mvua za El Nino Dk Mafuru amesema kwa sasa mvua hizo zimeshafikia asilimia tisini ya uwezekano wa kunyesha ingawa bado wanazifuatila kujua kama zinaweza zikaungana na zile za msimu wa vuli zinazotarajia kunyesha mwezi oktoba mpaka Disemba
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment