NA PAUL KAYANDA-KAHAMA
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Ushetu, Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga Gagi Lala ameisisitiza Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo chini ya mkurugenzi wake Hadija Mohamed kuendelea kutatua changamoto zilizopo ili kutenda haki kwa wananchi.
Pia ameitaka ofisi hiyo kuzingatia ushauri wa baraza la Madiwani kuzingatia changamoto ya ukusanywaji hafifu wa mapato chini ya asilimia miamoja na kutopeleka fedha kwa asilimia mia moja kwenye miradi ya maendeleo pamoja huku akisema kuwa kwa kuwa wanaanza upya wakawe makini sasa.
Aidha mwenyekiti huyo amesema kuwa pia katika Halmashauri hiyo ipo changamoto ya wakulima wa tumbaku nakutumia kikao hicho kuiomba serikali ihakikishe inalipa wakulima hao kwani ni haki yao.
Hata hivyo Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri hiyo Hadija Mohamed Kubonela amelihakikishia baraza hilo utekelezaji mzuri wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.
Hata hivyo kwa upande wake makamu mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Emmanuel Makashi akiwashukuru madiwani wenzake kwa kumchagua kurudi kwenye kiti chake amewataka madiwani hao kumpa ushirikiano ili waweze kutumikia vyema wananchi wa Ushetu.
Emanuel Makashi, diwani wa Kata ya Saba sabini halmashauri ya Ushetu akitoa shukrani zake kwa madiwani kumchagua kuwa makamu mwenyekiti
No comments:
Post a Comment