KUWASA YAJIVUNIA WATEJA WAKE KUWA WAMINIFU, YAWATAKA KUEPUKA VISHOKA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 2 August 2023

KUWASA YAJIVUNIA WATEJA WAKE KUWA WAMINIFU, YAWATAKA KUEPUKA VISHOKA

Afisa uhusiano mwandamizi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA) Manispaa ya Kahama, John Mkama akizungumza kwenye kipindi cha redio Huheso FM cha Morning Class leo Agosti 02, 2023.



NA MWANDISHI WETU-KUWASA


Leo tarehe 02/08/2023, Afisa Uhusiano Mwandamizi (PRO) wa KUWASA, John Matoke Mkama akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja (DCS), Eddymary Chimalilo wameendelea na zoezi la utoaji elimu kwa umma kupitia Redio Huheso FM masafa ya 104.5MHZ.

Mkurugenzi huduma kwa wateja wa mamlaka maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA) Manispaa ya Kahama, Eddymary Chimalilo kwenye kipindi cha redio Huheso FM Morning Class leo Agosti 02, 2023.


Maeneo ambayo yameongelewa na yamepewa kipaumbele katika kipindi kilichofanyika asubuhi cha Morning Class (Darasa la Asubuhi) ni pamoja na:-


1. Umuhimu wa wananchi kuendelea kushiriki katika dhana nzima ya kutunza na kulinda miundombinu ya maji.


Wito umetolewa kwa wateja kuendelea kutoa kipaumbelee katika kushirikiana na Mamlaka kulinda Miundombinu iliyopo kwa ufanisi na uendelevu wa huduma bora.
Afisa uhusiano mwandamizi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA) Manispaa ya Kahama, John Mkama akizungumza kwenye kipindi cha redio Huheso FM cha Morning Class leo Agosti 02, 2023.


2. Wananchi wamekumbushwa kuendelea na utamaduni wa kutenga bajeti kwa ajili ya huduma za maji hususani kwa ambao hawajaunganishiwa huduma hii.


Wito umetolewa kwa wananchi waendelee kujitokeza kuomba huduma kwa maana gharama zake ni nafuu huku msisitizo ukitolewa kwa wateja kuepuka kuwatumia *vishoka* ambao wamekuwa wakiwaongezea gharama kubwa za kuvuta maji.


Wananachi pia wameombwa waendelee kufuata taratibu za maunganisho mapya ya Maji zinazotolewa na KUWASA kwani ni rahisi na hazina gharama yoyote. Msisitizo umetolewa kuwa Mamlaka haiwatambui vishoka na wala sio mawakala na hawafanyi kazi kwa niaba ya Mamlaka. *EPUKA VISHOKA, OKOA GHARAMA*

Afisa uhusiano mwandamizi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA) Manispaa ya Kahama, John Mkama akizungumza kwenye kipindi cha redio Huheso FM cha Morning Class leo Agosti 02, 2023.


Kwa upande wa wateja wanaotumia huduma zetu wamesisitizwa kuendelea kulipa bill zao kwa wakati. Kwamba ili jambo hili lifanikiwe wito umetolewa kwa wateja kuendelea kutenga bajeti kwa ajili ya bill zao za kila mwezi kama wanavyofanya kwenye bajeti zingine za kawaida kama chakula na mambo mengine ya kijamii. 


Hii itawasaidia wateja kuepuka usumbufu wa kusitishiwa huduma na Mamlaka itakuwa kwenye nafasi nzuri ya kuendelea kutoa *Huduma Bora* kwa wateja wake huku ikiwa na uhakika wa kuendelea kupanua miundombinu ili kuwafikia wateja wengi zaidi.

Mkurugenzi huduma kwa wateja wa mamlaka maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA) Manispaa ya Kahama, Eddymary Chimalilo kwenye kipindi cha redio Huheso FM Morning Class leo Agosti 02, 2023.


3. *Rushwa* imekemewa sana na imesisitizwa kuwa malipo yote ya serikali yanafanywa kupitia *Control Number* na hivyo, KUWASA inatambua malipo yote yaliyofanywa kwa Control Number tu na si vinginevyo.


4. KUWASA imeahidi kuwa itaendelea kuwashirikisha wateja wote katika zoezi zima la kusoma mita zao ambapo wito umetolewa kwa wateja wote kuendelea kuwa tayari wanaposhirikishwa juu ya suala hili la usomaji mita na wanapotumiwa meseji (sms) za usomaji basi wachukue hatua mara moja ya kujiridhisha na taarifa ya usomaji husika ambapo wadau tumefahamishwa ratiba ya usomaji inayoanza kila mwezi tarehe 20 hadi tarehe 28.

Afisa uhusiano mwandamizi wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira (KUWASA) Manispaa ya Kahama, John Mkama akizungumza kwenye kipindi cha redio Huheso FM cha Morning Class leo Agosti 02, 2023.

Kwamba, endapo mita ya mteja haijasomwa kwa sababu mbalimbali ikiwemo mteja kutokuwepo nyumbani na geti kufungwa, wateja wameombwa kuwasiliana na KUWASA ili zoezi hilo lifanyike kwa wakati na kwa matokeo chanya.


5. *Wizi wa maji* nao umekemewa na wadau wamehimizwa kuendelea kuwa wazalendo kwa kushirikiana na Mamlaka katika kuwafichua watu wote wanaoiba au kuihujumu Mamlaka kwa namna yoyote Ile.


Hamasa imetolewa kwa wale wote watakaofanikisha ukamatwaji wa wezi, kuwa Mamlaka itaendelea kutunza siri zao na itaendelea kutoa motisha kwa wasiri (informers).


6. Vilevile, Wananchi wametakiwa kuendelea kuwa karibu zaidi na Mamlaka kwa maana ni chombo/taasisi yao, na watoe taarifa za mivujo kupitia namba za huduma kwa wateja na wajitokeze kuifutilia Mamlaka kupitia Mitandao ya Kijamii (website, Whatsapp na Instagram) kama sehemu ya kupata taarifa rasmi na kutoa maoni na ushauri wao kwa haraka zaidi kwa lengo la kuboresha huduma.


7. Kwa upande wa wananchi waliobahatika kupiga simu moja kwa moja, wameipongeza KUWASA kwa jitahada za utoaji elimu, huduma bora, uharaka wa kushughulikia changamoto za wateja na wametoa wito kuwa elimu kwa wateja iendelee kutolewa ikiwemo elimu ya matumizi ya mita iendelee kutolewa kwa wateja wote ili wateja waelewe namna *Mita za Maji/Dira* zinavyofanya kazi ili kuondoa manung'uniko kwa wateja hasa ukubwa na usahihi wa bill za maji lakini pia ili kuwafanya wateja waweze kulinganisha taarifa za usomaji na uhalisia katika mita zao.


Aidha wateja wamekubali kuwa wataendelea kutimiza wajibu wa kutoa taarifa za mivujo mara kwa mara ili kushirikiana na Mamlaka katika kupambana na upotevu wa maji huku wakiahidi kuwa wataendelea kulinda miundombinu.


Ombi/Rai imetolewa kwa Mamlaka ichukue hatua za haraka kwa baadhi ya wenye nyumba za kupangisha wenye tabia ya kuwauzia wapangaji wao maji kwa bei Kubwa ya zaidi ya sh. 200 kwa ndoo na kwa wale ambao wana rekebisha /*edit* bill za maji kwa lengo la kuwaongezea wapangaji wao bei ya maji nao washughulikiwe haraka iwezekanavyo


*KUWASA- JUHUDI ZETU, MAFANIKIO YETU*

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso