HALMASHAURI YA WILAYA MISSENYI YAPATA TUZO YA HALMASHAURI BORA MKOANI KAGERA KATIKA MAONYESHO YA KILIMO NANE NANE 2023 - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Sunday, 6 August 2023

HALMASHAURI YA WILAYA MISSENYI YAPATA TUZO YA HALMASHAURI BORA MKOANI KAGERA KATIKA MAONYESHO YA KILIMO NANE NANE 2023

Timu ya ushindi kutoka Halmashauri ya Missenyi


Baadhi ya maafisa kilimo,mifugo na uvuvi wakifurahia wakifurahia ushindi baada ya kupokea tuzo (kutoka kulia Mkuu wa Idara ya kilimo Tapita Tuvana Solomoni,Maengo Nchimani,Fatuma Yusuf,Vestina Kahangile na Hadija Kondo)


Halmashauri ya Wilaya Missenyi mkoani Kagera imepata tuzo ya halmashauri bora Mkoani hapa katika maonyesho ya kilimo nane nane yanayofanyika viwanja vya Kyakailabwa vilivyoko Manispaa ya Bukoba.


NA MUTAYOBA ARBOGAST-BUKOBA


Mbali na tuzo hiyo Halmashauri ya Missenyi (Missenyi Agri-Aqua) pia imepata tuzo ya mdau bora katika sekta ya uvuvi Mkoani Kagera.


Missenyi pia imekuwa mshindi wa pili katika maonyesho ya nane nane nyuma ya kiwanda Cha Sukari Kagera kilichopata nafasi ya kwanza ya mshindi wa jumla wa maonyesho ya nane nane mwaka 2023.


Tuzo zimekabidhiwa tarehe 5 Agosti 2023 na Mkuu wa Mkoa Kagera aliyewakilishwa na Mkuu wa Wilaya Bukoba Erasto Sima.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso