KAMISHNA wa kinga na tiba Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya nchini Dr. Peter Mfisi amesema kuwa wapo nane nane kwenye maonesho ya kilimo kwa sababu dawa za kulevya zipo za aina mbili kwamba kuna dawa za kulevya zinazotengenezwa viwandani kama heroin, kokein na dawa zingine lakini kuna dawa zingine zinatokana na kilimo kama bangi, Mirungi kwa hiyo ushiriki wao nane nane ni juu ya kuwaelezea wakulima kwamba wakati mwingine wasijihusishe na mazao hayo haramu kama bangi na mirungi.
Amesema kuwa pia wapo kuwaonyesha jinsi bangi inavyoonekana na kubainisha kuwa kuna baadhi ya watu ambao tumewahi kukuta mashamba makubwa yamelimwa wamepanda bangi humo wamechanganya na mazao mengine lakini majirani walisema kuwa wao walikuwa hawajui kama ni bangi na hawajui kama bangi ni zao haramu.
Mfisi amesema hayo baada ya kutembelewa kwenye banda lake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri mkuu,Sera, Bunge na Uratibu, Mhe. Ummy Nderinanga katika maonesho hayo ya nane nane jijini Mbeya.
Aidha amesema kuwa wananchi waliju kuwa hayo ni majani tu ya kawaida na hata walipo kuwa wakivuna walijua wanapalilia tu kuondoa magugu kwamana hiyo kupitia maonesho hayo anaamini wakulima wengi watakuwa na ufahamu mkubwa na kutojihusisha tena na kilimo cha mazao ya mimea ya dawa za kulevya kama vile bangi na mirungi.
''Hapa tunatoa elimu ya jumla juu ya madhara ya dawa za kulevya kwa sababu ukiangalia tangu tumeanza maonesho watu waliopita kwenye banda letu ni wengi sana wanafika 10,000 kwa hiyo idadi hiyo wamekuwa na uelewa kuhusu madhara yanayotokana na dawa za kulevya,'' alisema Mfisi.
Pia kiongozi huyo amesema kuwa moja ya mikakati ya mamlaka kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya ni kutoa elimu kwa jamii juu ya madhara yanayotokana na madawa ya kulevya ili jamii ijijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya.
No comments:
Post a Comment