KAIMU Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Nafaka na Mazao Mchanganyiko (CPB) John Maige amesema katika msimu huu wa kilimo tayari Bodi hiyo imeshanunua takriban tani 35,000 za mazao mbalimbali ya wakulima hapa nchini.
Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya John Mwakangale jijini Mbeya kwenye Banda ya Bodi hiyo ,Maige amesema miongoni mwa mazao yaliyonunuliwa ni pamoja na mahindi,mpunga ,alizeti na maharage .
Amesema mwaka huu Bodi hiyo imepanga kutumia takriban shlingi bilioni 100 huku akisema mpaka sasa tayari wameshatumia shilingi bilioni 29 huku akisema kazi hiyo ya kununua mazao bado inaendelea.
“Bado tunaendelea na ununuzi wa mazao ya nafaka katika vituo vyetu mbalimbali vilivyopo Iringa,Arusha Dodoma,Sumbawanga,Songea na Tunduma.”amesema Mkurugenzi
Ametumia nafsi hiyo kuwakaribisha wananchi kutemebelea banda la lao ili waweze kujionea na kujipatia bidhaa mbalimbali ambazo tayari zimeshaongezwa thamani na kuwa na ubora mkubwa.
Aidha amesema baada ya maonyesho hayo ,bidhaa hizo za CPB zinaendelea kupatikana katika ofisi zilizopo katika kanda za Nyanda za Juu Iringa,Kanda ya Ziwa Mwanza,Kanda ya Kaskazini Arusha , Kanda ya Kati Dodoma na Kanda ya Mashariki Dar es Salam.
Mkurugenzi huyo amesema mwelekeo wa Bodi hiyo ni kujiimarisha zaidi katika biashara kwa maana ya ununuzi wa mazao ya wakulima na kuyaongezea thamani na kuyauza katika masoko ya ndani nan je ya nchi.
“Bidhaa zetu tunazozalisha ni bora sana kwa sababu tunazingatia viwango vya ubora wa Afrika Mashariki tunazalisha unga wa sembe ulio bora kwa kutumia teknlojia za kisasa inayosindika bidhaa za unga wa mahindi ,unga ngano na hata mchele ,na kwa sababu ni taasisi inayozingatiwa viwango vya ubora vya Afrika Mashariki na Kimatifa ,bidhaa tunazolisha ni bora kwa ajili ya watumiaji na zinalinda afya za walaji.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Bodi ya CPB Nicomed Bohay amesema,CBP ipo kwa ajili ya kutatua changamoto ya soko kwa wakulima .
“Tunanunua mazao mbalimbali kwa wakulima ,lengo ni kutatua changamoto ya soko kwa wakulima ili wauze mazao yao kwa urahisi na hivyo kuwaongezea ari ya kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao mbali.
No comments:
Post a Comment