MJUMBE wa kamati ya Utekelezaji na Mbunge wa Viti maalumu katika Bunge la Tanzania, Subira Mgalu amekana bandari ya Dar es Salaam na maeneo mengine kuuzwa kwa kampuni ya Mwarabu inayozungumzwa kila kukicha na kwamba hakuna atakayeweza kuuza bandari hiyo.
NA PAUL KAYANDA-KAHAMA
Mgalu ambaye pia ni mjumbe wa Bunge la kamati ya bajeti akiwa katika ziara ya mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda pamoja na wajumbe wa NEC Mkoa wa Shinyanga amewataka wananchi wa Mkoa wa Shinyanga na Watanzania kwa ujumla kupuuza uzushi huo unaoenezwa na chama pinzani, na kuwahakikishia kuwa hakuna mtu atakayeweza kuuza bandari.
Mjumbe huyo amesema hayo wakati akizungumza na wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM Kata za Majengo, Malunga pamoja na Mhongolo kwenye mkutano wa hazara uliofanyika katika viwanja vya Maroli Kata ya Majengo Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga.
Kada huyo amesema kuwa hakuna atakayeweza kuuza bandari milele na milele na kuongeza kuwa bandari haiuziki kwa sababu lasrimali zake ni zaasili inayodumu mililele haiuziki na kwamba bandari hiyo imeanza kuendeshwa na mbia binafsi kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka jana.
Kada huyo wa CCM amesema kuwa hapa,Kahama ni wilaya ya Mwisho katika awamu ya kwanza ya Mikoa saba nchini lengo ni kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotelelezwa na Halmashauri mbalimbali za Wilaya na Mikoa, hususani fedha hizo zinazoletwa na Mh.Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.
“Kinachoendelea sasa, Tulichopitisha Bungeni Ule mkataba wala siyo mkataba wa utekelezaji, Ndiyo maana nimesimama kueleza kampuni ya DP WORLD haipo nchini pamoja na kwamba tumepitisha azimio kwa sababu gani ule mkataba ni wa mashirikiano baina ya Dubai na Tanzania katika masuala ya kijamii na uendeshaji wa bandari,” amesema Mgalu na kuongeza.
“Huwezi kuingia mikataba ya kimataifa kama hakuna mahusiano, ndiyo maana msingi wa mkataba ule baada ya wabunge kulidhia ndiyo mazungumzo yanaendelea, kuja kwenye mikataba ya uendeshaji,” amesema Mh. Subila Mgalu mjumbe wa kamati ya utekelezaji na mbunge wa viti maalumu.
Aidha Mjumbe huyo wa Kamati ya utekelezaji ya CCM amesema kuwa kuna chama cha siasa kinapita hakina ajenda, na kuwataka wantanzania wasidanganywe kuwa bandari imeuzwa na kuongeza kuwa kwenye mkataba huo yametajwa maeneo mahususi na bandari iliyotajwa ni Dare es Salaam na ile ya Kibaha, hakuna ya Tanga, Tanganyika wala Kanda ya Ziwa.
“Ni uongo kusema bandari zote na mkataba umesema watakapokuwa na mafanikio Face One ndio serikali ya Tanzania inaweza kupitia mamlaka ya bandari wakamwambia mbia Yule kuwa maeneo mengine unaonaje? Lakini wao wanatangaza uongo.
No comments:
Post a Comment