Serikali Wazazi/walezi na wadau mbalimbali wa maendeleo wametakiwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa lengo likiwa ni kuwalinda mabinti walioko kwenye hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kuwawezesha kufikia ndoto zao za kimaisha.
Na Taikile Tulo - Huheso Digital Iringa
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Halima Dendego akihutubia wageni na wadau katika kikao cha tathmini ya DREAMS Mkoa wa Iringa inayotekelezwa Manispaa ya Iringa na Mufindi.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Halima Dendego ambae alikua mgeni rasmi kwenye kikao cha tathimini cha shughuli za DREAMS kupitia mradi wa EpiC kilichofanyika leo julai 13,2023 kwenye ukumbi wa Sun Set Hotel katika manispaa ya Iringa kilichohusisha AGYW,Wazazi,wadau wa maendeleo na Taasisi za FHI360, HUHESO Foundation na TAHEA.
Amesema wazazi ni sehemu ya changamoto kwa baadhi ya mabinti ambapo wazazi wengi wamesahau majukumu yao ya kulea watoto wao na hivyo kuiachia mitandao kama vile Facebook na Instagram kuwalelea watoto jambo ambalo linapelekea mabinti wengi kujiingiza kwenye ngono na kupelekea mabinti hao kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi.
“Nina hakika,tukiendelea kuunganisha nguvu zetu hivi ,mabinti watanufaika kwa kupatiwa fursa mbalimbali na hatimaye kuweza kuwa na mabinti wanaojitambua,ushupavu,Wenye kujiamini,wasio na maambukizo ya VVU, Wazazi turudi kwenye desturi zetu kwa kufundisha, kukemea, kuadhibu mtoto anapokosea na kuwalinda watoto wetu”,Dendego alisema.
Aidha mkuu wa mkoa amesema hali ya maambukizi kwa Mkoa wa Iringa ni 11.3% hivyo ipo haja ya kufanya tathimini kushikamana kukubali kubadilika na kutokomeza maambukizi mapya ya VVU.
“Nimevutiwa sana na mradi wa EpiC unavyofanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na serikali katika utekelezaji wake hapa mkoani Iringa. Jitihada hizi za DREAMS ni mpango mzuri kwa ajili ya ukombozi wa mabinti wetu katika mkoa na hususani halmashauri zetu za Iringa Manispaa na Mufindi ili kuwakinga na maambukizi ya VVU na kuwawezesha kujitambua nakujilinda dhidi ya VVU/UKIMWI.
“Mahitaji ya mabinti walio katika rika hili ni mengi ambayo bila kushughulikiwa kikamilifu hakika mabinti hawa hawawezi kuwa salama kutokana na vishawishi wanavyokabiliana navyo”,Dendego alisema.
Dendego amesema serikali ipo pamoja na mabinti katika jitihada za kujikwamua katika changamoto mbalimbali zinazowakabili ,Serikali itaendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wadau ili kutafuta fursa na kujenga mazingira mazuri ili kuweza kuondokana na utegemezi na changamoto zinazo wakabili.
Hata hivyo Mkuu wa Mkoa amewapongeza wadau kutoka FHI360 pamoja na taasisi za HUHESO Foundation na TAHEA kupitia mradi wa EpiC kwa kuendelea kuchangia jitihada za Serikali ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufikia malengo ya kudhibiti maambukizi mapya ya VVU katika jamii yetu.
Naye Msitaiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mh. Ibrahim Ngwanda Amepongeza sana Wadau wote FHI360 pamoja na Huheso Foundation na TAHEA kwa jitihada za kuisaidia serikali kufikia malengo hasa kuwafikia mabinti kwenye Mkoa wa Iringa na Manispaa ya ya Iringa, hii inasaidia mabinti kwanza kujitambua na kuweza kujikinga na maambukizi ya VVU na Ukimwi, pia Mh Ngwanda ametoa wito kwa Serikali kuendelea kuwapatia ushirikiano wadau wote ili wawewze kutekeleza majukumu yao ili kufikia malengo ya mradi.
Msitaiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mh. Ibrahim Ngwanda akitoa neno katika kikao cha tathmini ya mradi wa DREAMS kilichofanyika Sun Set Hotel Manispaa ya Iringa
Kwa upande wake Chirstina Mafie Msimamizi wa DREAMS mkoa FHI360 amesema yapo malengo ambayo wanapaswa kuyafikia kwa mwaka ambapo wanatakiwa kufikia mabinti 4500 kwa Manispaa ya Iringa na mpaka sasa wamefikia mabinti 4000 sawa na asilimia 91,huku halmashauri ya Mufindi mabinti 11,000 na tayari wamefika mabinti 6000 sawa na asilimia 53 wenye umri wa miaka 15-17 kwa upande wa mabinti wenye umri wa miaka 15-17 kwa Manispaa ya Iringa wanatakiwa kufikia mabinti 1200 na tayari mpaka sasa wamefikia mabinti 800 sawa na asilimia 67 na kwa halmashauri ya Mufindi mabinti 2800 na tayari wamefikia mabinti 68 sawa na asilimia 28%.
Nae Mkurugenzi wa Shirika la TAHEA Mh. Lediana Mng’ong’o amewashukuru wadau wote na viongozi wote walioshiriki kikao hicho cha tathmini na kuwapongeza mabinti kwa kazi nzuri na kukubali kuwa sehemu ya mradi kwani bila wao mradi huu si chochote kwani DREAMS ina kazi ya kusaidia mabinti kujikwamua kiuchumi.
Mkurugenzi wa Shirika la TAHEA Mh. Lediana Mng’ong’o akizungumza na kuwashukuru wadau wote katika kusaidia mabinti katika Mradi wa DREAMS
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Huheso Foundation Juma Mwesigwa akitoa neno la Shukrani kwenye kikao cha tathmini ya Mradi wa DREAMS kilichofanyika Sun Set Hotel Manispaa ya Iringa
Mnufaika wa Mradi wa DREAMS Martha Victor akitoa ushuhuda jinsi ambavyo mradi wa EPIC kupitia dream ilivyomnufaisha katika maisha yake kwani ameweza kujikwamua kwa kilimo cha mbogamboga na kuweza kujipatia kipato
Meneja wa Mradi wa EPIC Mkoa wa Iringa na Njombe Ndugu Denis Bikaru (Kulia) akifuatilia kwa makini wakati wa kikao cha Tathmini ya DREAMS Mkoa wa Iringa inayotekelezwa katika Halimashauri ya Mufindi na Manispaa ya Iringa
Kaimu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mufindi Mh. Michael Kiliwa akitoa na nasaha kwa wadau na viongozi wa Serikali na kufunga kikao cha tathmini ya DREAMS mkoa wa Iringa kilichofanyika Sun Set Hotel Manispaa ya Iringa
Baadhi ya wadau na viongozi mbalimbali toka Serikalini walioshiriki kikao cha tathmini ya DREAMS Mkoa wa Iringa kilichofanyika Sun Set Hotel Manispaa ya Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Halima Dendego akiwa na baadhi ya Wadau wa Maendeleo akiwemo Meneja wa Mradi wa EpIC Mkoa wa Iringa na Njombe Ndugu Denis Bikaru aliyeketi mwanzoni Kushoto wakati wa kikao cha tathmini ya DREAMS Mkoa wa Iringa.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mh. Halima Dendego Katikati, Kulia kwake Kaimu Mwenyekiti wa Halmasahauria Mufindi Mh Michael Kiliwa akifuatiwa na Meneja mradi wa Epic Mkoa wa Iringa na Njombe Ndg. Denis Bikaru, Na kushoto ya Mkuu wa Mkoa ni Msitaiki Meya wa Manispaa ya Iringa Mh. Ibrahim Ngwanda na anayefuata na Mganga Mkuu wa Mkoa Dr. Mohamed Mang'una kwenye picha ya pamoja wakati wa kikao cha tathmini ya Dreams Mkoa wa Iringa.
Baadhi ya Washiriki wa Kikao cha tathmini ya DREAMS Mkoa wa Iringa kilichofanyika Sun Set Hotel Manispaa ya Iringa wakifuatilia kwa makini hotuba ya mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati akifungua kikao cha tathmini ya DREAMS Mkoa wa Iringa kilichofanyika Sun Set Hotel Manispaa ya Iringa.
Picha zote na HUHESO Foundation
No comments:
Post a Comment