Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Angellah Kairuki amewaagiza maofisa utumishi na makatibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu (TSC), kuhakikisha wanafuatilia walimu ambao hawajapandishwa vyeo kwa muda mrefu.
Maagizo mengine ni kuhakikisha kuwa madai ya walimu wote ikiwemo malimbikizo ya mishahara yanaingizwa katika mamlaka husika na kufuatilia madai ya malimbikizo ya fedha za likizo na uhamisho.
Kairuki ametoa maagizo hayo leo Jumatano Julai 5, 2023 wakati akifungua kikao cha maofisa utumishi wa wilaya na makatibu wa TSC wa wilaya zote Tanzania Bara.
soma zaidi:https://www.mwananchi.co.tz/mw/habari/kitaifa/waziri-kairuki-atoa-maagizo-matatu-kutatua-kero-za-waalimu-4293650
No comments:
Post a Comment