MWENGE WA UHURU WATUA SHINYANGA KUKIMBIZWA KILOMITA ZAIDI YA MIA TANO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 27 July 2023

MWENGE WA UHURU WATUA SHINYANGA KUKIMBIZWA KILOMITA ZAIDI YA MIA TANO



Mkoa wa Shinyanga umepokea mwenge wa uhuru rasmi leo ukitokea mkoani Simiyu.


Ambapo mwenge huo ukiwa mkoani Shinyanga utakimbizwa umbali wa kilomita 571.5 na kuifikia miradi 41 yenye thamani ya Sh. bilioni 41.02.


Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Christina Mdme amesema katika Miradi hiyo, Miradi 11 itawekewa Mawe ya Msingi, 14 itazunduliwa, Minne itafunguliwa, na Miradi 12 itaonwa.


Amesema Miradi hiyo imegharamiwa na Serikali kuu Sh. bilioni 8.7 Halmashauri Sh. bilioni 3.9, nguvu za wananchi Sh. milioni 116.4, Sekta binafsi na wahisani mbalimbali Sh. Bilioni 1.2.


Aidha, ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, wajitokeze kwa wingi kuupokea Mwenge huo ambao utakuwa ukipita katika maeneo yao na kwenye miradi.


Mbio hizo za Mwenge wa Uhuru mkoani Shinyanga zinaanza kukimbizwa katika wilaya ya Kishapu kwa kuzindua, kuweka mawe ya msingi na kuona jumla ya miradi 6 yenye thamani ya Sh.bilioni 1.3.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso