WAWEZESHAJI MABINTI KIUCHUMI 18 WAWEZESHWA VITENDEA KAZI NA HUHESO FOUNDATION - IRINGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 2 June 2023

WAWEZESHAJI MABINTI KIUCHUMI 18 WAWEZESHWA VITENDEA KAZI NA HUHESO FOUNDATION - IRINGA

Katibu tawala msaidizi menejimenti rasilimali watu wa Mkoa wa Iringa Mh Deogratius Yinza amewaasa viongozi wa serikali, wadau wa maendeleo na wawezeshaji mabinti kiuchumi (Mentor) kufanya kazi kwa uwazi ili kuwezesha mabinti wananufaika na afua ya Determined Resilient, Empowered, AIDS-free Mentored and safe (DREAM) inayotekelezwa na Mradi wa EpiC.


Na Taikile Turo - Huheso Digital Blog Iringa

Katibu Tawala msaidizi Menejimenti Rasilimali watu wa Mkoa wa Iringa Mh Deogratius Yinza akiongea na viongozi wa Serikali na wadau katika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa wa Iringa wakati wa hafla ya ugawaji baiskeli kwa wawezeshaji mabinti kiuchumi (Mentor)



Wito huo umetolewa leo tarehe 02 June 2023, kwenye hafla ya ugawaji baisikeli kwa wawezeshaji mabinti kiuchumi(Mentor) iliyofanyika kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa iliyohudhuriwa na viongozi wa serikali, dini wadau wa maendeleo na wawezeshaji mambinti kiuchumi.


Amesema ni wajibu wa Serikali kufanya kazi kwa kushirikiana na wawazesha mabinti Kiuchumi ili waweze kufanya kazi zao kwa ufasaha na kuweza kufikia lengo la kusaidia mabinti wenye umri wa miaka 15-24 walio katika hatari ya kupata maambukizi ya VVU na kujikwamua kiuchumi.


Mradi wa EPIC unaotekelezwa na Shirika la FHI 360 kwa ufadhili wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa kukabiliana na UKIMWI (PEPFAR) Pamoja na shirika la Marekani la maendeleo ya kimataifa (USAID) una lengo la kuchangia jitihada za Serikali kufikia malengo ya kidunia ya kudhibiti janga la ukimwi na athari zake kwa jamii kwa kufikia malengo ya 95% tatu, ambapo walengwa wa mradi ni kuyafikia makundi mbalimbali yaliyopo katika mazingira hatarishi ya kuambukiza na kuambukizwa VVU na Ukimwi.


Mkurugenzi wa HUHESO FOUNDATION Ndugu. Juma Mwesigwa alisema “kama shirika tumelenga kuwainua mabinti kiuchumi kwa kupitia Mradi wa “Dream” kwa kuwagawia vitendea kazi hivyo ambavyo vitaenda kuwasaidia kuwafikia mabinti wengine wenye umri kati ya miaka 15 - 24 na waliopo katika vikundi na kuwapa elimu bora zinazo husiana na ukatili wa kijinsia sambamba na maambukizi ya VVU na virusi vya UKIMWI”

Kwa upande wake Lilian Ibrahim ambae ni mnufaika wa afua ya Dream amelipongeza Shirika la The Foundation for Human Health and Social Development (HUHESO Foundation) kwa kutekeleza mradi wa EpiC ambao umewasaidia mabinti wengi kujifunza masuala ya uzazi wa mpango,ukatili wa kijinsia na kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.


Gregory, Mariagloria ambae ni afisa msimamizi wa mabinti (DREAM) Shirika la HUHESO Foundation amesema mpaka sasa wamefanikiwa kuunda vikundi 159 vyenye jumla ya mabinti 3,008 waliojiunga na vikundi vya akiba na mikopo ambao mpaka sasa wamefanikiwa kuweka shilingi milioni kumi na tisa laki nane sabini na saba elfu, mia saba hamsini, na kutoa jumla ya mikopo 1,036 yenye thamani ya Tshs Milioni thelathini na thelathini na sita elfu mia tisa hamsini na kuweza kutengeneza faida yenye thamani ya Tshs Milioni mbili laki nne thelethini na mbili elfu na mia moja na kumi iliyotokana na riba za mikopo hiyo.


Aidha Meya wa Manispaa ya Iringa Ibrahim. A. Ngwanda ameahidi serikali kupitia ofisi za kata watashirikiana kuhakikisha wawezeshaji mabinti kiuchumi wanatumia baisikeli walizopewa wanazitumia kwa matumizi yaliyokusudiwa na kuwaasa kuendelea kuwasaidia mabinti kujikwamua kiuchumi.


Mstahiki Meya Wa Halmashauri Ya Manispaa ya Iringa Ndugu IBRAHIM NGWADA akitoa neno la Shukrani kwa Serikali na Wadau kuwafikia Mabinti na kuwapa vitendea kazi ili kuwafikia mabinti wengi zaidi katika Manispaa ya Iringa

Katibu tawala msaidizi menejimenti rasilimali watu wa Mkoa wa Iringa Mh Deogratius Yinza akikabidhi Baikeli kwa Mwezeshaji mabinti Dheridh kutoka kata ya Mivinjeni Manispaa ya Iringa.


Mkurugenzi wa HUHESO FOUNDATION Ndugu. Juma Mwesigwa akiwa na katika picha ya pamoja na wawezeshaji mabinti wakati wa hafla ya ugawaji baiskeli kwa Mawezeshaji mabinti kiuchumi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Iringa.

Katibu tawala msaidizi menejimenti rasilimali watu wa Mkoa wa Iringa Mh Deogratius Yinza akikabidhi Baikeli kwa Mwezeshaji mabinti Hadija H. Nuni kutoka kata ya Kihesa Manispaa ya Iringa.

Katibu tawala msaidizi menejimenti rasilimali watu wa Mkoa wa Iringa Mh Deogratius Yinza akikabidhi Baikeli kwa Mwezeshaji mabinti Valentina Chaula kutoka kata ya Kitwilu Manispaa ya Iringa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso