Waumini wa parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Njema , Mbulu, jimbo Katoliki la Kahama wamechanga kiasi cha shilingi milioni 26.6 mifuko ya saruji 119 na tofari 500 ili kuwajengea nyumba ya kukaa Mapadri wanaofanya kazi yao ya utume hapo waweze kuishi sehemu nzuri.
Na Patrick Mabula , Kahama.
Akiongea katika harambee ya kuchangia ujenzi wa nyumba Alexander Kazimil aliyechangia kiasi cha shilingi milioni 7 alisema wameamua kuwajengea nyumba ya kuishi mapadri kutokana na iliyopo kupitwa na wakati kwa sababau ilijengwa toka mwaka 1921 wakati parokia hiyo ilipofunguliwa.
Kazimil na familia yake aliyetoa mchango kiasi cha fedha hizo taslimu aliwashukuru waumini kwa moyo wao wa kuitikia wito wa mpango huo na kuunga mkono mradi katika kuwajengea nyumba mpya mapadri , pamoja na uzio wa parokia ili kulinda eneo hilo ambalo limekuwa likivamiwa na watu.
Paroko wa parokia hiyo Padri Joseph Sekere amewapongeza waumini kwa moyo wa kuamua kuanza ujenzi wa nyumba mpya ya kukaa waweze kukaa katika mazingira mazuri kutokana na iliyopo, kuwa ya zamani na ilijengwa toka mwaka 1921 zaidi ilipofunguliwa na wamisionari wa kizungu waliofika Africa kueneza injili.
Padri Sekere alisema moyo na ukarimu huo ni kuuitika wito wa Kristu katika moja ya kazi ya Mungu katika kuitegemeza kanisa kwa hali na mali ili watumishi wake waondokane na changamoto ya kukaa katika nyumba ya zamani yenye zaidi miaka 100 toka kufunguliwa kwa parokia hiyo mwaka 1921.
Naye mgeni rasmi katika harambee hiyo Benjamin Ngayiwa na kusindikizwa na ndugu na jamaa zake ambako kwa upande wake waliweza kuchangia zaidi ya kiasi cha milioni sita na kuwashukuru waumini wa parokia hiyo kwa moyo walionyesha wa kujitoka katika kushiriki kazi ya Mungu ili mapadri waweze kukaa sehemu nzuri wanapowatumikia.
Parokia ya Bikira Maria Mama wa Shauri Jema , Mbulu jimbo Katoliki la Kahama ilifunguliwa mwaka 1921 wakati huo ikiwa chini ya Jimbo kuu la Tabora ambapo nyumba ya kuishi mapadri imepitwa na wakati ambapo waumini wameamua kujitoa kujenga nyumba ya kisasa ya kuishi watumishi hao wa Mungu na kuweza kuanza kuchanga kiasi cha sh.26.6 milioni mifuko ya saruji 119 na tofari 500.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment