Wadau mbalimbali wakiwemo wandishi wa habari na wahariri wameiomba serikali kutunga sheria ya kuwanusuru watoto wa kike na mila kandamizi katika jamii hasa ukeketaji kwa wanawake na wasichana.
Ombi hilo limekuja baada ya kufanyika kikao kazi cha wahariri na wandishi wa habari kutoka vyombo tofauti vya habari nchini ikiwemo wa Luninga (TV) kilichofanyika April 27-28, 2023 wilayani Tarime mkoani Mara chini ya shirika la C-SEMA ambalo linafadhiliwa na UNFPA.
Katika warsha hiyo imebainika kuwa ukeketaji kwa wanawake na wasichana kwa sasa umevuka mipaka ambapo watoto wa kike na wanawake unapofika msimu wa mila hiyo ya ukeketaji huvushwa nje ya nchi ili kwenda kukeketwa hali ambayo inahatarisha afya zao.
Valerian Mgani kutoka FGM-Masanga kituo cha kuhifadhi wasichana na wanawake wanaokimbia ukeketaji amesema kuwa wanapokea kesi nyingi kila mwaka na hulipotiwa vituo vya polisi na kupelekwa mahakamani lakini zinashindwa kumalizika kutokana na kukosa ushahidi wa kutosha.
Valerian Mgani akiwaelezea wandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari namna ambavyo ukeketaji unaovuka mipaka ya nchi unavyofanyika.
Valerian Mgani akiwaelezea wandishi wa habari pamoja na wahariri wa vyombo vya habari namna ambavyo ukeketaji unaovuka mipaka ya nchi unavyofanyika na namna wanavyokabiliana na changamoto za kuzuia ukatili huo.
Amesema wamekutana na wandishi wa habari katika kikao kazi hicho ili kuwapa uwezo wa kuibua na kuelimisha jamii namna ya kuachana na mila kandamizi kwa wanawake na wasichana ili kuwanusuru na madhara ikiwemo kupoteza damu nyingi ambayo inaweza kupelekea kifo.
Mgani amesema ukeketaji umevuka mipaka ambapo kwa Mkoa wa Mara ambao uko jirani na nchi jirani ya Kenya msimu wa ukeketaji wanawake huvushwa mpakani kutoka Tanzania kwenda Kenya kutokana na jamii ya kabila la Kikurya kuwa na mwingiliano wa kiutawala wa kimila.
”Wasichana na wanawake huvushwa mipaka wale wa Kenya huja Tanzania na wale wa Tanzania hupelekwa Kenya ili kukeketwa na Mangariba kitu ambacho kinasababisha kwa kiwango kikubwa ukeketaji kushindwa kuisha”.
“Tunaiomba serikali ya Africa Mashariki katika hali hii kuna maazimio ambayo yaliadhimiwa na nchi tano za Uganda, Ethiopia, Somalia, Kenya na Tanzania kuyatekeleza ipasavyo ili kufikia 2030 mila ya ukeketaji iwe imekwisha”.
Michael Marwa, afisa miradi kutoka shirika la C-SESMA akizungumzia namna ya kuandika habari ambazo zitakuwa chachu ya kuelimisha jamii kuachana na ukeketaji.
Michael Marwa, afisa miradi kutoka shirika la C-SESMA akizungumzia namna ya kuandika habari ambazo zitakuwa chachu ya kuelimisha jamii kuachana na ukeketaji.
Afisa miradi wa shirika la C-SEMA, Michael Marwa amesema maazimio yaliyofikiwa April 2019 bado hayajashughulikiwa inavyopaswa kwani kuna baadhi ya nchi ambazo ukeketaji unatajwa kuwa mkubwa kama Somalia yenye asilimia 98 haina sheria ya kupinga mila hiyo.
Amesema Somalia bado wanajiendesha kwa mfumo wa sera hali ambayo kesi nyingi za ukeketaji kushindwa kumalizika na wanaohusika kuendelea kuwa huru hivyo nchi tano zote zinapaswa kutunga sheria mahususi ambayo watu wanaobainika wanachukuliwa sheria.
Marwa amesema ushahidi mara nyingi umekuwa ukipotezwa kutokana na kukosekana kwa sheria inayopinga ukeketaji japo kesi hizo zimekuwa zikishughulikiwa kwa sheria ukatili wa kijinsia hali inayowapa mwanya watu wote wanaobainika kutochukuliwa kwa hatua kali zaidi.
Kwa upande mkaguzi msaidizi wa Polisi Sirari, Cloud Mtweve amesema changamoto kubwa wanayokutana nayo katika kesi hizo ni watu muhimu wa kutoa ushahidi kwa wazazi au Mangariba waliohusika na kushinikiza mtoto wa kike au mwanamke kukeketwa kushindwa kutoa ushahidi.
Mtweve amesema kukosekana kwa sheria za moja kwa moja zinazowabana watu wanaojihusisha na ukeketaji zinatoa mwanya kwa jamii kuendekeza mila hiyo kandamizi.
Mkaguzi msaidizi wa jeshi la polisi kituo cha Sirari mkoani Mara, Cloud Mtweve akiwaelezea wahariri na wandishi wa habari namna ambavyo wanakabiliana na Mangariba wa ukeketaji
Aidha wandishi wa habari na wahariri wamejengewa uwezo wa kuandika habari za utafiti ambazo zitailinda jamii, wahanga na watu ambao wanapinga ukeketaji sambamba na uelimishaji wa jamii wa kuachana na desturi kandamizi kwa baadhi ya watu au makundi fulani.
No comments:
Post a Comment