NIMEDHAMIRIA KUMSAIDIA RAIS GEORGE WEAH KATIKA UONGOZI WAKE WA AWAMU YA PILI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 26 May 2023

NIMEDHAMIRIA KUMSAIDIA RAIS GEORGE WEAH KATIKA UONGOZI WAKE WA AWAMU YA PILI

 

 Jewel Howard Taylor


Utangulizi:Mh. Dk Jewel Howard Taylor, Makamu wa Rais, Jamhuri ya Liberia ni kito adimu(rare gem), ambaye nguvu zake kisiasa ni kama mti mkubwa usioweza kuangushwa kwa kifaa butu.Alikuwa mama wa taifa (first lady) la Liberia tangu mwaka 1997 hadi 2003, Seneta(mbunge) mwandamizi katika Bunge la Liberia, akiwakilisha kaunti ya Bongo ambako alifanya vyema chini ya uongozi wa chama cha Liberia People. 


Ni mwanamke wa kwanza nchini Liberia kupata wadhifa wa Makamu wa Rais. Mhariri mkuu wa Jarida la Chama cha waandishi habari Afrika (Congress of African Journalists’ CAJ Intl magazine), Michael Adeboboye, anafanya mahojiano na mh Howard Taylor, kama inavyotafsiriwa na Mutayoba Arbogast, kwa Kiswahili kutoka Kiingereza.


Taylor, anazungumzia siasa za Libera kwa jumla, Afrika, mtazamo wake kimaisha, ndoa yake na aliyepata kuwa Rais wa Liberia, Charles Taylor hadi kupewa talaka, anavyomuunga mkono George Weah anayegombea urais wa Liberia kwa muhula mwingine.


Mahojiano:

Nikiangalia baadhi ya mahojiano yako,hebu nnichukue mojawapo ya Januari 19, 2023, ambapo katika majibu yako ukiwa kituo cha redio LNTV 89.9 ulijidhihirisha kuwa mtu makini na Mkiristo dhabiti,anayejua nini maana ya upendo na kuwa na hofu ya Mungu; mama na mke anayejua kipi kinahitajika katika kujenga familia imara na kuwalea watoto na wajukuu.Mh kuna kitu kinakosekana katika mtazamo huo, au wewe ni mtu makini usiye na doa lolote?


Ukweli ni kwamba mimi si mtu nisiye na doa wala malaika.Hakuna mtu mkamilifu.Lakini kama ningeangalia mbele zaidi ya swali lako kwa kipimo cha 1 kwa kumi,ningejipa alama 8.ningesema kwa utetezi kwamba mi ni mwanamke mwenye roho nzuri,mwenye hofu ya Mungu, ambaye kwa namna ninavyoamini, nimebaki katika kuwapambania wanawake kwa kipindi cha zaidi ya miaka 20 kuhusu elimu, siasa, na uwezeshwaji kiuchumi.


Hii ni kwa neema ya Mungu.Naamini kwamba ni mfano wa kuigwa kuwa raia mwema.Naendelea kuwa mlezi wa wana na wajukuu.Napambana kuwa mtumishi mwaminifu wa shughuli za kijamii – nikifanya niwezavyo kutoa fursa kwa wanawake (kazi ambayo nimekuwa nikiifanya kwa zaidi ya miaka 20); nikiwa mwaminifu na rafiki mwenye dhamira.


Nikirudi kwenye swali lako la msingi:Nimewahi kufanya makosa katika maisha yangu? NDIYO, namna wanaume wote wanavozaliwa na mwanamke.Makosa hayo yanaweza kuathiri maamuzi yangu,au kunichagulia mimi ni nani? HAPANA. 


Hii ni kwa sababu ninayo dira kuu inayoniongoza kila hatua. Ingawa nimejikwaa na kuanguka mara nyingi; najua kuwa vikwazo ni kama mawe ya kupandia katika kujifunza na kuwa mwenye busra zaidi.Kitu kibaya ni kwamba,katika maisha kama ilivyo sasa, wanawake ndio wanahesabika kuwa na makosa kuliko wanaume katika mazingira yaleyale yanayofanana.


Tuangalie mifano hii. (a). Baadhi ya lawama ninazotupiwa mii ni kuwa ati nina baadhi ya marafiki wasio na maadili. Nataka niseme kuwa katika safari ya maisha kila mtu hukutana na watu wengi ; wabaya; wazuri;wasio na sura; wanaovutia; wenye akili; watu wa chini; waoga; mashujaa; marafiki wa maisha na wale wa muda.Wigo huu mzima unaungwa na picha mbalimbali zinazoweza kuakisiwa na kioo katika maisha ya mtu (Kaleidoscope).


Mwaka huu ninatimiza umri wa miaka 60, miaka iliyobaki kuishi ni michache kuliko hii. Matokeo yake nimekutana, kushirikiana na kusaidiana na watu mbalimbali labda wanaozidi hata 30,000.


Picha inayoweza kujitokeza ni kuwa – katika safari yangu kama nimekutana na watu watatu wanne wenye kutiliwa mashaka,au wametuhumia kwa kosa moja au jingin - ni halali kweli kunihukumu maisha yangu yote, licha ya mambo makubwa ya maendeleo niliyofanya kwa wengi hasa wanwake ulimwenguni, ndio nichukuliwe kuwa mwanamke anayestahili kuhojiwa mwenendo wake muda huu katika historia ya maisha yangu? 


Naamini kwamba huu ni msukumo tu wa wale watu ambao wanataka kunipima mimi ni nani. Maoni yangu ni kuwa, maisha ya mtu yanasibishwe na jumla ya matendo, na siyo tuhuma za chuki, kwamba, kwa sababu nilikuwa na marafiki ambao walikuwa au hawakuwa ‘raia wema’ – inamaanisha mimi si msafi bali naigiza tu !


Mh. Jewel Howard Taylor akiwa na Makamu wa Rais wa  Nigeria Prof. Yemi Osibanjo


Maisha yangu yamekuwa kitabu cha wazi tangu nilipokuwa mama wa Taifa(Fist Lady) in 1997 hadi sasa,na naamini kumbukumbu zinazungumza kwa niaba yangu.


Sheria zinazoilinda jamii yetu inatutaka kuwa na ustaarabu kwa msingi mkuu ”Watu wote watahesabika kuwa hawana hatia hadi pale itakapothibitika kuwa na hatia”, na pia hakuna mtu atashtakiwa kwa makosa ya wenzake.Nadhani wanaotaka kunidogosha (kunifanya mtu mdogo) zaidi ya nilivyo, wanakosea. 


Ninao marafiki wengi, wenye ujuzi wa mambo na wengineo, ambao ambao huteta mara kwa mara ; lakini hebu niruhusu kusafisha hali ya hewa mara hii, kwamba shughuli nilizonazo zenye kuleta mabadiliko chanya (siyo kwa wanafamilia tu) bali katika jamii pana, zinahusika kueleza maisha yangu.Historia hii chanya haiwezi kufutwa.


Mimi ni mwanamke wa kawaida mwenye matamanio ya kufanya yaliyo ndani ya uwezo wangu kuleta mabadiliko na matokeo chanya kwa kizazi change hasa kwa wanawake duniani,na kuacha alama ya mafanikio.Kama mwanamke,nimepambana na changamoto mbalimbali, kukatishwa tamaa,hasara,lakini na mafanikio pia .Nimemwaga machozi na kucheka pia nikihisi moyo wangu kupasuka kwa furaha. 


Nimepata uzoefu wa tamu na chugu, nimepitia mabonde na milima, lakini kupitia yote hayo,kwa huruma na uwezo wake Mwenyezi Mungu, nimeishi miaka 60 yenye mafanikio ya majitoleo yaliyozaa matunda,na thamani ya moyo wangu ilivyo na thamani ya utu wangu maishani inaonekana.


Ninatumaini na kuomba kwamba mahojiano haya yataweka wazi ukweli halisi wa maisha yangu na kuonesha wazi kwamba uvumi na uzushi vimetengenezwa maalum kutaka kuua historia yangu inayoonesha kwamba mimi ni mwanamke mwenye nguvu Afrika, ikidhaniwa kwa kufanya hivyo watakuwa wameitumbukiza historia hiyo kwenye chombo cha kutupia taka.


Lakini hali hii inanikumbusha Utenzi ulioandikwa na Maya Angelou-I RISE, ambao nimekuomba uuchape kwa wasomaji: “You may write me down in history with your bitter, twisted lies, You may trod me in the very dirt but still, like dust, I’ll rise.Does my sassiness upset you? Why are you beset with gloom? Cause i walk like I’ve got oil wells pumping in my living room. 


Just like moons and like suns, with the certainty of tides, just like hopes springing high, still I’ll rise. Did you want to see me broken? Bowed head and lowered eyes? Shoulders falling down like teardrops, weakened by my soulful cries? Does my haughtiness offend you? Don’t you take it awful hard’ cause i laugh like I’ve got gold mines digging’ in my own backyard.You may shoot me with your words, You may cut me with your eyes, You may kill me with your hatefulness, but still, like air, I’ll rise. 


Does my sexiness upset you? Does it come as a surprise that i dance like I’ve got diamonds at the meeting of my thighs? Out of the huts of history’s shame i rise Up from a past that’s rooted in pain. I rise i’m a black ocean, leaping and wide, welling and swelling i bear in the tide. Leaving behind nights of terror and fear i rise into a daybreak that’s wondrously clear. 


I rise bringing the gifts that my ancestors gave. I am the dream and the hope of the slave. I rise I rise I rise.” (“Unaweza kuandika historia yangu kwa ukali na uongo, unaweza kunikanyaga katika uchafu, lakini bado, kama lilivyo vumbi bado nitatimka.Utundu wangu unakuhangaisha? Kwa nini umetawaliwa na chuki? Kwa sababu natembea kana kwamba chumba changu kina visima vya mafuta. Kama ilivyo mwezi na jua, uhakika wa mawimbi, kama ambavyo matumaini huwa juu, nami nitainuka. 


Unataka kuniona nimevunjika moyo? Kichwa kilichoinamishwa na macho chini? Mabega yanayoshuka kama machozi ya mbwa,nikidhoofishwa na kilio cha moyo wangu? Mwenendo wangu unakutaabisha? Usijali sana maana nacheka kama vile kuna machimbo ya dhahabu ugani kwangu. Unaweza kunichoma kwa maneno yako,kuniumiza kwa macho yako. 


Unaweza kuniua kutokana na chuki yako,lakini kama hewa vile, nitainuka.Uzuri wangu unakutesa? Ni ajabu kwamba nacheza kama vile nina almasi kati ya mapaja yangu? 


Nje ya historia ya aibu, nainuka kutoka ukale uliojikita kwenye maumivu. Nainuka, mimi ni bahari nyeusi, nikikata mawimbi, naruka juu na kutanuka. Nikiacha nyuma usiku wa kihoro na hofu, nainuka wakati wa mchana,na hilo ni dhahiri shayiri. Ninainuka kuleta zawadi walizonipa mababu. Mimi ni ndoto na matumaini kwa walioko utumwani.Ninainuka, ninainuka,ninainuka”)

Mh. Jewel Howard Taylor akiwa na mh. Josephine Nkrumah,Mwakilishi mkazi wa Rais wa  Tume ya ECOWAS (Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi) nchini Liberia


Umekuwa ukizungumzia juu ya uhuru na uimara wa wanawake.Nini maoni yako juu ya hili kwa ujenzi wa taifa kwa mtazamo wa kiAfrika

Kwa majaaliwa yake Mungu, kama wengi walivyokuwa kabla yangu, nashukuru kuwa mmojawapo katika jambo hili – mwanamke huru, jasiri na mwenye maono na mfano wa kuigwa na mamilioni ya wanawake.Wale ambao niko juu kutokana na msaada wao; mama;wanangu; ndugu,; Bibi Ellen Johnson Sirleaf na Winnie Mandela, walinifundisha namna ya kukabiliana na ulimwengu kwa damu, jasho na machozi, ikiwa ni ishara ya ustahimilivu katika maisha.Ujumbe wao ulikuwa rahisi na na unaoeleweka –KUWA NA NDOTO,SIMAMA IMARA, PANGILIA, UFANISI, RUDISHA FADHILA KWA JAMII NA WASHAURI WENGINE.


Wazo hili la kutoangalia nyuma na badala yake kuangalia mbele hadi ndoto yako itakapotimia kwa kufanikiwa maono yako juu ya wanawake wote ulimwenguni, wasijiruhusu kukatishwa tama na kubaki dhalili .Lazima tutumie machozi yetu na maumivu ya mwili na akili tukibaki kuwa imara ili kusonga mbele kwa maana kuna mengi nyuma, na yanayotusubili mbele kuyatimiza.


Hii ndiyo ndoto yetu, matamanio na matarajio yetu ambayo kwayo yamejengwa kwa matofali imara kuwasaidia wanawake wajitambue,na wahesabiwe katika kuchangia vilivyo katika maendeleo ya jamii bila kujali aina ya vikwazo vinavyowakabili.


Hii ndiyo habari muhimu kwa mwanamke wa Afrika anavyotakiwa kuwa; ni mazingira gani yanayomzunguka?; wamefanya nini kwa miaka mtawalia na wameacha kumbukumbu gani. Kujua haya nijuayo sasa, nawapa heko kila mmoja wao (wa kale na wa sasa), kwa sababu hawa ndio mashujaa wa Afrika. Nikiwahusia wengine, endelea kutembea,songa mbele,endelea na ujenzi wa taifa,na macho yako yaangaze upeo wa macho ukiwa na Imani kuu.LOO! ni urithi uliotukuka!


Kufuatia jitihada zako juu ya kumwezesha mtoto wa kike na mwanamke, unayaonaje mafanikio ya Afrika kuhakikisha wanawake wanawezeshwa,hususan katika uwanja wa siasa?


Naam, yako mengi ya kujivunia kwani Afrika imetoka mbali, kutoka kuwafungia akina mama vyumbani hadi kuwaruhusu angalau wasikilize,kuwaruhusu kupaza sauti zao,kuwaruhusu kushiriki siasa, na leo,katika sehemu mbalimbali kuwaruhusu kuanza kuongoza.


Ukweli ni kwamba ingawa tunakwenda mbele, lakini ni mchakato unaokwenda taratibu,ingawa kwa miaka 25 mengi yamebadilika na tunajivunia hayo.Ndoto yetu ni kuwa siku moja, tena karibu tu, halitakuw tena jambo la mjadala hapa na pale,wala kuwashawishi wanaume waweze kuelewa, au kuwabembeleza kutufanyia hisani kwa jambo ambalo ni haki yetu, lakini nchi zote za Afriks zitakuwa kama ilivyo Rwanda hii leo. 


Siku hiyo itachukuliwa kwa ujumla kuwa ndio mwenendo wa maisha,Jinsia zote mbili kufanya kazi pamoja katika kudumisha amani na maendeleo endelevu ulimwenguni.


Hata hivyo, nakubali kwamba ili mchakato huu ufanikiwe unahitaji nguvu za pamoja za wanawake. Ni mchakato wa pamoja kama zilivyo mbio za kupokezana vijiti. Wale wanaotambua yaliyombele yetu na wamedhamiria kufanya kazi, siyo kwamba hadi wachoke, bali pale watakapobadili uelekeo na kuunadi umuhimu wa wanawake katika safari hii, na watakaosalia katika mbio hizi ni wale waliojizatiti kufikia lengo. 


Bado kuna mengi ya kufanya hadi ndoa za utotoni na ukeketaji vimepigwa marufuku na nchi zote (kwani mtindo huu wa ukeketaji unaendelea katika nchi zilizoendelea za kimagharibi), hadi pale jinsia zote mbili zitakapopewa umuhimu sawa na bila unyanyapaa kutokana na desturi, hadi pale minyororo iliyowafunga wanawake itakapokatwa kabisa.Tumedhamiria kuhakikisha hilo.


Binafsi, ningesema kwa uwazi kuwa wewe ni mwanamke shupavu, ukitokea katika msingi wa ndoa yako kwa mbabe wa vita Charles Taylor,hadi kuwa seneta kwa vipindi viwili katika nchi ya Liberia yenye mfumo dume, na sasa kuwa Makamu wa kwanza wa Rais ambaye ni mwanamke. Katika siasa kuna changamoto nyingi utakazokutana nazo kadri munavyoendelea kupanda ngazi,unaweza kutuambia baadhi ya changamoto hizo na namna unavyokabiliana nazo?


(Akitabasamu ) ….jibu la swali hili litabaki katika kumbukumbu hivi karibuni.Ingawa, nikieleza kwa ufupi, kwamba uzoefu katika maisha yangu umenifanya kuwa JEWEL OF AFRICA(Tunu ya Afrika),kama wanavyopenda kuniita. Inasemmwa kuwa ili dhahabu iwe safi au almasi yenye thamani lazima vipite kwenye tanuru la moto .


Huu ni muhtasari wa maisha yangu,ingawa habari ya maisha yangu haina upekee kwangu tu.Ni moja kati ya habari za wanawake shupavu na wenye mafanikio. Changamoto hizi huwakumba wanawake wote wenye tamaa ya mabadiliko kuelekea maisha bora, na wale walio tayari kubadili mienendo hasi katika jamii, kutoka kuwa na upendeleo, ubaguzi, fursa adimu, ukatili wa kijinsia, ukosefu wa wadhamini na washauri, dhana potofu, upendeleo wa kitamaduni na jadi, kutoaminiana, na juu ya yote – unyanyasaji uliokubuhulakini kwa njia za hila; unyanyasaji wa kiakili na kutengwa na wakati mwingine lugha za chuki, mambo ambayo yanatuathiri. Wakati mwingine nashangazwa na namna tunavyojibu.


Lakini baadaye unajifunza namna ya kukabiliana na tatizo ukiwa umelenga mbele na kudhamiria ,ukichukua hatua bada ya nyingine,bila kukata tama huku ukitabasamu.Ni rahisi? HAPANA.Ila ndicho hiki hutufanya kuwa wanawake.Tunaendelea hatua kwa hatua, kizazi baada ya kizazi, na taratibu lakini kwa uhakika,tunafanikiwa mmoja baada ya mwingine.


Mh, ukitafakari juu ya kupata talaka, unaweza kuitaja ndoa yako na aliyekuwa Rais wa Liberia na mbabe wa kivita,kuwa kilikuwa kipindi cha giza?


Kwa kulitambua suala hili baadaye, naweza kusema ndoa yangu na Charles haikuwa ya kawaida kutokana na kupitia vipindi na nyakati za vita vya wenyewe kwa wenyewe na machafuko. 


Ila swali linakuwa gumu kidogo unapoongeza maneno-mbabe wa kivita na kipindi cha giza. Inaashiria kuwa alikuwa mtu jahili na kiumbe katili, na mtu anakwenda mbali kwa kuuliza hivi kwa nini alikubali kuolewa naye? Utahitaji kusubiri kitabu cha historia yangu (Biography) kitakapokamilika. 


Lakini ngoja niseme kwamba nilipokutana na Charles, hakuwa mbabe wa vita wala kiumbe katili.


Ninavyomuona kwa upande mwingine,Charles Ghankay Taylor,niseme kwa upande mmoja alikuwa mtu mwenye mvuto,baba wa kutumainiwa,tafiki mwaminifu na kiongozi anayejali, miongoni mwa mengi. 


Upande wake mwingine, wakati wa ile miaka yake ya vita kabla ya kuwa Rais wa Liberia,ni habari inayoweza kuhadithiwa na wale waliokuwa sehemu ya mapambano. 


Sikuwa sehemu ya awamu hii ya maisha yake,na siwezi kusimulia kile ambacho sikukiona. Huenda ukauliza tena,kama hivyo ndivyo kwa nini ulimtaliki? Jibu jepesi – WIVU. 


Kwa kuwa kulikuwa na bibi Taylor wengi na katika mazingira hayo, yule mjanja na mwingi wa mahaba alikumbatiwa. Nilipotea njia na sikujua vipi naweza kujiweka sawa, kwa hiyo nilijiondoa kwenye mzingo wake na kuishi maisha yangu katika mazingira ya kuchanganyikiwa, uchungu na maumivu makali.Baada ya muda, bila kuona matumaini mbele, nilifanya uamuzi mgumu wa kupata talaka, kuweka mipango ya ndoto zangu na kutengeneza njia yangu na kuifuata hadi mwisho kuzima mazongezonge.


Ni wazi kuwa,kwa haiba na badhi ya maoni ya viongozi wanashangaa kwa nini unaendelea kutumia jina la aliyekuwa mme wako hata baada ya talaka, na wengi wanahisi (iwe sahihi au la) kwamba, ni ubinafsi, umekwishamtaliki, unatumia jina lake kwa maslahi ya kisiasa ili uweze kufika nafasi ya juu.Ungependa kusema nini juu ya hili?


Nasema maoni hayo hayana msingi na wala si kweli.Unaona, kuna bibi Taylors wengi hapa, Kila mmoja amechagua njia yake ya kuishi kwa namna anavyofanya. Mimi kwa upande wangu nimedhamiria kuwa wakala wa mabadiliko chanya,na nimefanya hivo kwa bidii. Matunda ya kazi hiyo ni kuwa na Liberia moja yenye WANAWAKE HODARI. Kazi yangu na matokeo yake,dhamira na utashi vimeliinua jina hilo na wala halikutupwa kwenye tope.Ni jina nililochagua tarehe 31 Januari 1997. 


Niliulizwa swali na ripota maarufu wa BBC, Bi Elizabeth Blunt kwamba – Baada ya kuolewa na Charles Taylor ,ungependa kuitwaje? Nilisema ningependa kuitwa JEWEL HOWARD TAYLOR. 


Na hilo ndilo limekuwa jina langu tangu wakati huo. Kwa wale wanaofikiri natumia jina hilo kupata umaarufu au ni hisani, wanatakiwa kuangalia pande zote mbili za sarafu. Sababu moja ni kuwa mimi ni mwanasiasa wa kike maarufu. Iwapo ningebadili jina langu, kungetokea nini kwa mafanikio niliyojenga kwa miaka mingi kwa kudra zake Mungu? Ningekuwa sitambuliki tena, na ingebidi nitoe maelezo kila wakati 


kudhihirisha kuwa sikuwa mtu bandia.Kwa kuwa nimejenga utambulisho huo maalum – JEWEL HOWARD TAYLOR, Ni rahisi kunitambua mimi ni nani katika ngazi zote. Kwa maana ukisikia jina hilo, unajua ni mimi kiuhalisia na si mwingine yeyote. Ingawa kuna akina Taylors wengine (bandia na halisi), nashukuru mi ndiye Jewl Howard Taylor pekee. Sababu nyingine ni kwamba natembelea nyota yake?


Ukweli ni kwamba ukiangalia Mungu alivyonijalia toka ngazi moja hadi nyingine,utaona kwamba nimetengeneza njia yangu mwenyewe na napita humo. Ningewza kuwa mama wa Taifa au la. Nilichagua kuwa hakuna kitu muhimu kama kulitumikia Taifa,niliishinda dhoruba na kusonga mbele kuutumikia umma. 


Kwa hiyo leo kwa neema na huruma yake Mungu,nimempanda farasi wangu mwenyewe, hasa ukizingatia kuwa chaguo mlangu ilikuwa niwe Gavana wa Benki kuu.Nadhani sikuwa na mfupa wa uaanasiasa mwilini. Lakini kwa jinsi nilivyoweza kishinda hofu ya kutokujulikana, na kuchagua kuwa mwanasiasa mwenye kuleta mabadiliko chanya ambayo kila mzalendo hufanya kwa nafasi yake, nilitafuta njia yangu/farasi wangu (ushauri na uanaharakati kwa wanawake kisiasa na nguvu za kiuchumi), na kuungana na wengine katika mabadiliko haya muhimu kwa ustawi na maendeleo ya nchi pendwa ya Liberia. Safari imekuwa ngumu na yenye viunzi, ila ndiyo safari yangu, ingawa wengine wangetamani kuniangusha (MUNGU APISHILIE MBALI). 


Nashukuru kuwa wako maelfu WANAOTHAMINI NINACHOFANYA na wananipongeza. Ila naweka akilini tafakari kama yalivyo maneno ya wimbo wa zamani kuhusu moyo wa Mnegro (old Negro soul song) ,”Kuna mbio nazostahili kukimbia, kuna ushindi natakiwa nishinde,Mungu nipe nguvu kila saa, kuwa mwaminifu kwa mbio hizi” (“there is a race, that i must run, there are victories to be won, give me power Lord, every hour, to remain true to run this race”)



Ngoja nielekeze mazungumzo yetu kuhusu uchumi wa Afrika, nakummbuka katika mkutano mmoja nchini Afrika kusini, wakati fulani mwezi Desemba 2022.Uliziomba nchi za Afrika na wafanyabiashara kuwekeza katika bara hili.Kumekuwa na utayari gani katika kulitekeleza hili?

Naamini kwamba Afrika haijafika kwenye kilele cha mafanikio.Kuukubali mkataba wa biashara huru (Free Trade Agreement) ni dalili kwamba kuna mwamko mpya wa KiAfrika (African Reinaissance), ambao aliyekuwa Rais wa Afrika kusini, Thabo Mbeki, aliuzungumzia miaka 30 iliyopita. Aliitaka Afrika kujitafakari, kuwa na imani, kuwajibika kwa nguvu zote kuleta mwamko mpya. Mimi ni muumini wa wazo hilo kwamba Afrika ifanye kila iwezalo kuwa bara lenye nguvu kwa njia iliyo sahihi. Leo jitihada zinafanyika kuondoa hali ya upendeleo na vizuizi vingine,ishirikiane na wadau wa maendeleo ndani ya bara la Afrika ambalo kwa miaka 10 ijayo litakuwa na idadi kubwa ya watu na huku likliendelea kumiliki kwa asilimia 50 ya raslimali zote ulimwenguni. Ni jambo la muhimu kwamba viongozi wa nchi za Afrika kuunga mkono Agenda hii ya KiAfrika,agenda itakayoifanya Afrika kuwa huru kutoka kwenye utumwa wa kiuchumi, ili kuwawezesha vijana wetu wawe na matumaini na kutuamini tena.



Kiwango kikubwa cha vijana wasio na ajira hapa Afrika ni cha kutisha.Nchini Liberia vijana ni 70% na wengi wao hawana ajira.Serikali yako inakabilianaje na hali hii?


Vijana ni watu muhimu katika kukua kwa maendeleo ya nchi yoyote ile. Wanawakilisha PANDE MBILI ZA UPANGA. Upande mmoja, wanapoachwa bila ajira, wanaweza kutumika katika kuhatarisha amani na kudhoofisha maendeleo ya nchi yetu. 


Kwa upande mwingine wakiwezeshwa na kuajiriwa wanakuwa injini ya kukua ,uvumbuzi na mageuzi katika nchi.Katikati ya agenda ya nchi yetu ya Kupambana na umaskini kwa ajili ya ustawi na maendeleo (Pro poor Agenda for Prosperity and Development-PAPD),tulionesha MADARAKA NI YA WATU na UCHUMI na AJIRA ili kukabiliana na ukosefu wa ajira. Kwa kutumia mkopo kutoka Benki ya dunia (World Bank), wa Dola za Marekani milioni 10 na tukatekeleza kwa mafanikio mradi wa Fursa kwa Vijana (Youth Opportunities Project-YOP) uliolenga kusisimua uchumi wa vijana lengwa. Mradi ulilenga vijana 15,000 kuanzia umri wa miaka 15-35, ambao asilimia 50 ni wale jinsia ya kike walio katika mazingira magumu.


Mradi ulilenga stadi za maisha na ujasiriamali,matumii ya vifaa na fursa katika kilimo cha pamoja,ambapo wengi wa washiriki walitoka maeneo ya vijijini. Msaada huu uliwawezesha kuwa na ajira zenye tija, na kujihusisha pia na shughuli nyinginezo zinazoinua uchumi wao, na pia kuchangia katika maendeleo ya jamii zao.


Mheshimiwa Rais George M. Weah alizindua mradi wa Dola za Marekani 22 milioni tarehe 31 Machi 2022, zilizotolewa na Shirika la maendeleo la Marekani, USAID kwa ajili ya mradi wa kuwaendeleza vijana (Youth Advance Project). 


Mradi huu unalenga kuwawezesha vijan 21,000 katika majimbo ya Montserrado, Bassa na Lofa kupitia elimu na stadi za msingi ili kuboresha maisha na uzalishaji mali.Ikumbukwe kuwa,awali Rais alishazindua mradi mwingine tarehe 14 Januari 2022 wa Shughuli za mageuzi ya kiuchumi kwa sekta binafsi mili ijiajiri (Recovery of Economic Activity for Liberia Informal Sector Empowerement-REALISE) wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 10 kutoka Benki ya dunia na serikali ya Ufaransa,kuwawezesha vijana 19,000 walio katika mazingira magumu kupambana na umaskini kwa kujiajiri binafsi. Tunayo mipango mingi katiak seikali ya kupambana na ukosefu wa ajira kwa vijana katika sekta kuu mtambuka za afya, elimu, jinsia na kilimo.Tunaendelea kulipa uzito mkubwa suala hili la ukosefu wa ajira kwa vijana na tumedhamiria,kwa kushirikiana na marafiki zetu washirika,kuendelea kupambana nalo.



Iwapo unaweza kutathmini ufanisi wa serikali ya Liberia,unadhani wananchi wanataka nini katika uchaguzi ujao?

Katikati ya changamoto,serikali yetu ilirithi uchumi unaochechemea kwa kushuka uwekezaji wa moja kwa moja toka nje (Foreign Direct Investment) kupitia UNMIL, kuondoka kwa mashirika makubwa ya kimataifa (NGOs) na kiwango cha kutisha cha kukata tama kwa wafadhili. Matukio haya yalidhihirisha ukweli mkwamba kwa zaidi ya miaka 10, Liberia ilikuwa ikiishi kwa amani na ikiwa imara, na hivyo ijitayarishe kumiliki tena uchumi wake. Tulitambua changamoto hizi tangu siku ya kwanza na tukaanza kufanya kazi na Shikrika la Fedha Duniani (IMF),kutusaidia kujenga uchumi mdogo mdogo na kupunguza mfumko wa bei.


Tulisawazisha na kuoanisha malipo ya mishahara, kupunguza matumizi, na kubuni mbinu mpya za kuongeza fedha kwenye miradi ya maendeleo.Kupitia kuheshimu matumizi ya fedha na kupanua wigo wa fedha,tuliongeza uwezo wa mapato ya ndani ambayo yalichangia katika bajeti yetu iliyofikia Dola za Marekani 794.5, bajeti kubwa katika nchi iliyotoka kwenye vita. Mpaka hapa kiukweli najivunia yale tuliyotekeleza, ukizingatia athari za Covid 19 na mgogoro wa kiuchumi. Kuna ongezeko la kujivunia katika Elimu, Afya, Kilimo,Jinsia, miongoni mwa sekta nyinginezo. Kwa mfano, katika sekta yetu ya Nishati katika kueneza umeme nchi nzima hali imeanza kuimarika, shukrani kwa kuweza kununua umeme wa ziada kwa msaada wa ECOWAS Power Pool. 


Katika Afya, taratibu katika majimbo zinaimarika, baadhi ikiwa ni Ujenzi wa hospitali yenye vifaa kikamilifu kwa ajili ya Jeshi (the 14 Military hospital), kunapia ile hospitali mpya kabisa yenye vifaa toshelezi, ya Emirates, iliyoko Gbarpolu, tunajivunia sasa kufungua kwa mara ya kwanza tangu nchi itoke kwenye hali ya vita, Kampuni ya utengenezaji dawa (Pharmaceutical Manufacturing Company), na tunaendelea na juhudi za kuweka vifaa JFK na hospitali zote za serikali nchini. Tumeboresha pia mishahara ya madaktari pamoja na manesi na watumishi wengine wa afya. 


Katika sekta ya elimu tumeanzisha sera ya masomo ya ziada yasiyolipiwa katika ngazi za juu kwenye shule za serikali, malipo ya karo ya wanafunzi wa WASSCE kwa darasa la 12 (12 graders) nchini kote,kujenga na kuwezesha vifaa katika taasisi za TVET ncchini kote na pia ujenzi wa shule za wanafunzi wenye mahitaji maalum.


Kwa ujumla, najivunia mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa, na dhamira ya washirika wetu kutusaidia zaidi.Rais George Weah atabeba ujumbe huu wa mafanikio nchi nzima wakati akitafuta ridhaa ya kuchaguliwa kwa mara nyingine tena. Hii ni kumbukumbu kuhusu serikali yetu.


Hata hivyo, ukiangalia ukweli nchi nzima,unatarajia uungwaji mkono wa wananchi wa Liberia kuturuhusiwa kuongoza, kutokana na kazi nzuri tuliyofanya.



Wewe ni kiongozi wa Seneti ya Liberia, umechagukiwa katika Seneti mara mbili kabla ya kuwa Makamu wa Rais, kwa hiyo una uzoefu mara mbili katika shugfhuli za kiutendaji na Bunge.Je, kwa hakika unaona mhimili wa sheria katika nchi za Afrika unaisimamia serikali kutimiza wajibu wake katika kuhakikisha mizania sawa ya kiutendaji,ukizingatia matumizi mabaya ya madaraka?

Hili ni swali la kati ya kuku na yai kipi kilitangulia.Lakini naamini kwamba Bunge katika nchi yoyote,hususan nchi za Afrika, ni walinzi (custodian) wa MADARAKA NI YA WATU, na kuna kuwajibika endapo mambo hayatakwenda kwa dira sahihi. Katiba za nchi zote zinatoa haki na wajibu katika kulinda uhuru na matumizi ya madaraka. Swali halisi lingekuwa-Kwa nini inaonekana kana kwamba haifanyiki katika mazingira mengi? Huenda kunahitajika kufanya tathmini na ripoti juu ya jambo hili ili kuweza kupata jibu,na kusambaza ripoti hiyo kwa nchi zote za Afrika.Waone katiba zao zilivyo na namna wanavyoweza kubadilisha mambo. 


Kwa hakika huu utakuwa ni wajibu mkubwa kwa wote. Bara letu linahitaji raia wazalendo ambao watafanya kazi na wakuu wa nchi na mahakama kuijenga Afrika yenye usawa na ustawi.


Afrika inayo amana ya kutosha ya maliasili pamoja na raslimali watu, unafikiri ni kwa nini bara hili linaendelea kujikokota nyuma kimaendeleo hususan katika eneo la uchumi, na kitu gani Afrika inatakiwa kufanya?


Nchi za Afrika zikazanie kuwa na umeme wa uhakika, kufungue milango ya kiuchumi, kuondoa vizuizi vya kiuchumi baina yao, kuwekeza katika teknolojia na ubunifu, na kutafuta njia nzuri zaidi za usafirishaji na huduma bora,miongoni mwa mengi, yote muhimu katika ujenzi wa mwamko mpya wa Kiafrika. Vilevile tuhimize kutafuta suluhu kwa matatizo yetu, huku tukitafuta njia muafaka ya kuwaleta Waafrika popote walipo dunian i(diaspora) kusaidia kuijenga Afrika.



Mh. Unazungumzaje juu ya hili, “Makamu wa Rais wa sasa wa Liberia, Bi Jewel Howard Taylor,hajawahi kuwa mbali na mabishano na utata kabla ya kupanda hapo juu alipo,kwanza akiwa Seneta wa Kaunti ya Bongo na baadaye Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Liberia”


Nadhani utata ( mzuri au mbaya) ni sehemu ya siasa.Wanaume wanalikwepa hili? HAPANA.Inakuwaje kwangu na kisha kutenda kwamba hali hiyo inabainisha maisha ya mtu ya baadaye?Kwa hakika katika kitabu maarufu 48 Laws of Power by Robert Green – kuna sehemu chini ya Kanuni namba 6 isemayo, “Umuhimu wa mahakama kwa gharama yoyote”, Inaendelea kusema kuwa –sifa mbaya (notoriority) ya aina yoyote ni sifa nzuri. 


Na ni vizuri zaidi mtu kusingiziwa na kushambuliwa kulikon kupuuzwa. “Unaona, kwa wanawake wengi, tumefunzwa kuwa kimya, usijulikane, usilete chokochoko, baki kuwa mwanamke. Bali siasa haitaki kuwa na moyo laini ila kuwa na moyo wa samba, kwa hiyo kutakuwa na utata mwingi, mwingi tu, kadri mtu atakavyokaa ofisini, na naamini kwamba wale wanaomfahamu Jewel Howard Taylor halisi, watakuwa wanafahamu zaidi. 


Kwa hiyo sitahofia zaidi kelele hizo,shutuma, uongo na chuki, naendelea na hatua zangu nikiangalia mbele katika kutimiza dhamira, wajbu na ndoto zangu.


“Mwaka 2022 wananchi wa Liberia walishangazwa na taarifa zilizosambaa toka Obi Cubana hadi Sheik Bassirou Kante – zikieleza kuwa Makamu wa Rais, Taylor, ulitajwa kujihusisha na watu waliodhaniwa kuwa makundi yanayojihusisha na utakatishaji fedha” kama ilivyotajwa katika Ripoti. Mh. Unaweza kusemaje juu ya kuhusishwa na watu hao kwa suala hilo linalotajwa?


Kama nilivyosema mwanzo,k kuna baadhi ya watu ambao hupenda kuamini mambo hasi, kwa sababu za kijicho ,husuda na chuki, naniajuaye? Kiukweli nimekutana na watu wa kila aina katika kipindi chanu cha uongozi, na jinsi ninavyosonga mbele, nina imani nitakutana na watu wa haiba tofauti tofauti. Lengo langu ni kuendelea kuwa imara moyo wangu ukisalia kwenye njia msahihi, kufanya kazi kwa bidii, na nisiruhusu kitu chochote kiwe kizuri au kibaya, kuniondoa kwenye lengo langu. Muhimu ni kwamba hizo ni tetesi zisizo na ukweli.



Kulingana na Ripoti ya Mahakama ya Marekani (United State Court) iliyofichua kwamba Makamu wa Rais Jewel Howard Taylor alikuwa na urafiki wa karibu na Sheik Bassirou Kante ambaye alikamatwa na serikali ya Marekani kwa tuhuma za utakatishaji fedha na kuingilia mifumo ya kielektroniki, jambo lililowashangaza wengi, pia gazeti la FrontPage Africa lilifichua habari kwamba milionea wa Nigeria, Obi Cubana alikamatwa nchini Nigeria mwezi Novemba 2021 muda mfupi baada ya kurejea kutoka Nigeria, ambapo iliripotiwa alikuwa na mazungumzo kuhusu Ushirikiano wa kibiashara na Makamu wa Rais, Bi Taylor.Unaweza kutupatia mwanga juu ya suala hili?


Sina uhakika urafiki wangu binafsi na Sheik Bassirou Kanye una maana gani, lakini nilikutana naye kwa njia ya kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahitaji.Wananchi wa Liberia pamoja nasi tulishirikiana katika miradi mbalimbali. 


Urafiki wetu ulikuwa ni kuwasaidia wale wahitaji mwasiojiweza, na haukwenda zaidi ya hapo.Kama vile ambavyo baathi ya watu wanasingizia kwamba nilikuwa na uhusiano wa kimapenzi naye – hilo ni mbali na ukweli. Tajiri Obi Cubana alikuja Liberia kwa mara ya kwanza akitafuta fursa za biashara katika sekta ya utalii. 


Alikuwa mmojawapo katika ujumbe wa kibiashara wa watu wengi waliokuwa na mawazo sawa ya kibiashara. Nikiwa sauti mojawapo iliyojiandaa kuwaonesha fursa nyingi za kibiashara nchini Liberia, nilikutana na ujumbe huo na kuuonesha kuwa Liberia ina fursa kubwa za uwekezaji, Naamini kila mzalendo andechukua nafasi hiyo kuitangaza nchi, na kuvutia wawekezaji na kuwa na ushirikiano halali kusaidia kuimarika kwa uchumi wa Nigeria.


Tafadhali tueleze, ungependelea kugombea urais pamoja na George Weah kama Makamu wake wa Rais, au ungependa kuchukua njia nyingine ya kisiasa?


Nimedhamiria kujitolea kikamilifu kumuunga mkono Rais George Manneh Weah katika juhudi zake za kutafuta mhula wa pili, na najitahidi kadri niwezavyo kufanikisha jambo hili. Nathibitisha kuwa namuunga mkono Rais Weah kwa nguvu zangu zote.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso