Mkazi wa mtaa wa Nyasubi wilayani Kahama mkoani Shinyanga Mseveni Mchele (35-40) anashikiliwa na jeshi la Polisi kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wake wa kufikia mwenye umri wa miaka 12 Mwanafunzi darasa la saba shule ya Msingi Nyasubi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza na waandishi wa habari leo Ijumaa Aprili 7,2023.
Na Salvatory Ntandu - Kahama
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amethibitisha kukamatwa kwa Mseveni na kudai kuwa Jeshi la Polisi wanaendelea na upepelezi wakikamilisha atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili.
Alisema kuwa kitendo alichokifanya Mchele ni kiyume na maadili ya Kitanzania kwani haiwezekani baba kumbaka mwanae hata kama hajamzaa,na kuwataka wazazi na walezi kutokengeuka na badala yake watimize wajibu wao katika Malezi bora ya Watoto.
“Katika hili jeshi la Polisi mkoa wa Shinyanga hatutakuwa na mhali kwa mtuhumiwa kwani kitendo alichonya sio cha kiungwana haiwezekani baba kubaka mwanae tutahakikisha hatua kali za kisheria zinachukuliwa kwake ili iwefundisho kwa watu wengine,’alisema Magomi.
Naye Afisa ustawi wa jamii Manispaa ya Kahama Abrahaman Nuru alisema kuwa baada ya Mseveni kukamatwa walilazimika kumpeleka hospitali mwanafunzi huyo kwa ajili ya vipimo ambapo daktari alibainisha kuingiliwa.
“Mseveni baada ya maafisa Ustawi kumkamata alikiri kutenda kosa hilo kwa madai kuwa ulevi ndio umemsababishia kufanya kosa jambo lililosababisha kumpeleka kituo cha polisi Kahama kwa taratibu za kisheria,”alisema Nuru.
Kwa upande wake Mhanga wa tukio hilo ambaye jina lake limehifadhiwa alikiri kubakwa na baba yake wa kambo kwani alikuwa anamletea Chipsi na Kimiminika cheupe chenye asili ya Kilevi ambacho alikuwa anamlazimisha kunywa kwa madai kuwa ni dawa ya kutibu ugonjwa wa UTI.
“Wiki mbili zimepita baada ya Mama yangu kusafiri kwenda mkoani Morogoro kwenye matibabu baba amekuwa akinipa vimiminika hivyo na kujikuta nimelewa na nipo chumbani kwake nikiwa nimevuliwa nguo,”alisema Mhanga wa ukatili.
Hata hivyo Mama mkubwa wa Mhanga wa ukati huo ambaye hakutaka jina lake litajwe alisema kuwa taarifa za kubakwa kwa binti huyo zilitolewa na majirani zake baada ya kusikia kelele usiku za mwanae kufanyiwa ukatili huo na baba yake wa kambo ndipo walipotoa taarifa kwa ustawi wa jamii Kahama.
“Kwa sasa nimemchukua mwanangu wakati tunamsubiraia mama yake atoke kwenye matibabu mkoani Morogoro,kitendo alichokifanya baba yake wa kambo hakifai na tunaiomba serikali ichukue hatua kali za kisheria ili iwe fundisho kwa wazazi wanaowafanyia ukatili watoto wao,”alisema Mama mkubwa mhanga wa ukatili.
CHANZO:MALUNDE 1 BLOG
No comments:
Post a Comment