Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Siima amewataka wananchi katika halmashauri ya Bukoba(Bukoba vijijini) kuilinda fedha yote inayopatikana kwenye mauzo ya maji na kuiweka benki ili miradi ikiwa na tatizo iweze kufanyiwa matengenezo haraka.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba, Erasto Siima akiwa katika uzinduzi miradi ya maji Bukoba Vijijini(Halmashauri ya Bukoba)
Na Mutayoba Arbogast,HUHESO DIGITAL BLOG, Bukoba
Akizungumza na wananchi wa kijiji Omkiisi kata Kyamlaile na Kijiji Karonge kata ya Ibwera wakati akizundua miradi mipya ya katika vijiji hivyo, Mh Siima amesema serikali ya Rais Dkt samia Suluhu Hassan inatumia fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwamo ya maji hivyo wananchi hawana budi kuilinda dhidi ya uharibifu ili iweze kuwahudumia kwa muda mrefu.
Amesisitiza juu ya umuhimu wa wananchi wananchi kusomewa taarifa ya mapato na matumizi kila baada ya miezi mitatu katika kuweka uwazi na uwajibikaji ili miradi ya maji iwe endelevu huku Jumuiya za maji zikitakiwa kukaa mara kwa mara ili kutambua mapema matatizo yanayoweza kujitokeza.
Akitoa taarifa ya upatikanaji wa maji katika halmashauri ya Bukoba, Meneja wa Ruwasa katika halmshauri hiyo Mhandisi Evaristo Mugaya amesema kuwa shilingi bilioni moja na milioni 274.8 zimetumika kuwajengea miradi ya maji wakazi wapatao 14,800 katika kata za Ibwera ,Katoma,Kibirizi na Kyamlaile ambapo miradi hiyo imekamilika kwa asilimia 100% na wananchi wanaendelea kupata huduma.
Mhandisi Mugaya ameitaja miradi hiyo kuwa ni Karonge,Kashenge-Irogero,Omkihisi na Kibiriz ambapo vituo 37 vya kuchotea maji vimejengwa kwa ajili ya wananchi huku kukamilika kwa miradi hiyo kumeongeza upatikanaji wa maji katika halmashauri ya Bukoba kutoka asilimia 68 hadi 74 hadi sasa.
Amefafanua kuwa kupitia kwa wakala wa maji vijijini wanatarajia kuchimba visima virefu 12 katika maeneo ya Ruhunga,Nsheshe,Kishogo,Kashule,Rukoma,Izimbya,Katoro,Kaibanja,Musira,Mgajwale,Kasharu,Kuhumlo na miradi yote hiyo itagharimu shilingi milioni 682.4
Aidha ameongeza kuwa Ruwasa Bukoba imepanga kuanza ujenzi wa miradi ya maji katika vijiji vya Mulahya,Buganguzi,Minazi,Katoju,Bulinda na Maruku kupitia mradi wa Kemondo- Maruku awamu ya pili na ujenzi wa miradi ya maji Migara,Kikomelo-Butakya,Mushozi,Kasharu na Bumai kupitia mpango wa Programu za matokeo(Programme for Results-P4R), ambapo mpaka sasa taratibu za manunuzi zipo hatua ya mwisho na ujenzi wake unataraji kuanza mapema mwezi April 2023.
No comments:
Post a Comment