Walimu wanachukulia mtaala mpya wa elimu nchini Kenya kwa uzito huku wakitumia njia yoyote kuwafundisha watoto wao.
Mwalimu mmoja amemiminiwa sifa kutoka na ubunifu wake wa kuwasomesha wanafunzi. Mwalimu huyo alimleta ng'ombe darasani ili kuwasaidia wanafunzi wake kuweza kuelewa zaidi
Katika video hiyo iliyosambaa, alitumia ng'ombe halisi kuwafunza wanafunzi wake, ambao walikuwa wamejawa na mshawasha wakati wa somo lake.
Mwalimu huyo alikuwa nyuma ya darasa huku wanafunzi wakitaja sehemu za ng'ombe walizoweza kuona.
Ng'ombe huyo mweupe alisimama mbele ya darasa akiwa ametulia tuli huku watoto wakimkazia macho wakati wa kipindi hicho.
Wakati mmoja, alifikiri alisikia wakitaja ng'ombe na mikono na kuwauliza wanafunzi kama wanyama wana mikono.
Walimsahihisha haraka na kusema, “ulimi” huku wengine wakigeuka nyuma kumwangalia jinsi walivyojibu.
TAZAMA VIDEO
Katika taarifa sawia na hiyo, video ilisambaa ya mwalimu akiwafundisha wanafunzi sehemu za mwili wa samaki.
Kwenye video hiyo kwenye Twitter, mwalimu huyo mwenye bidii alionekana kuwa mtu wa kujieleza wakati akielezea sehemu tofauti za samaki.
Alisimama mbele ya darasa, akiwa amemshikilia samaki mikononi mwake na kumtumia kama nyenzo ya kufundishia kwa wanafunzi.
Aligeuza samaki kutoka upande mmoja hadi mwingine akielekeza kwenye sehemu za mnyama huyo wa majini ili kuboresha ufundishaji wake.
Wanamtandao waliguswa na dhamira yake hiyo na kusema mshahara wa mwalimu unapaswa kuongezwa kwa kuwa anafanya kazi nzuri.
CHANZO:MALUNDE 1 BLOG
No comments:
Post a Comment