MANESI SABA WA USIKU MBARONI KWA KUKUTWA NA DAWA KWENYE MIKOBA YAO YA MKONONI KAHAMA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 7 March 2023

MANESI SABA WA USIKU MBARONI KWA KUKUTWA NA DAWA KWENYE MIKOBA YAO YA MKONONI KAHAMA


picha ya mfano wa dawa ambazo hazihusiani na wauguzi kukamatwa na nazo

Jumla ya Wauguzi/Manesi saba katika hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga wamefikishwa kituo cha polisi Kahama baada ya kudaiwa kuwauzia wagonjwa dawa usiku wa manane.




Wauguzi hao wanadaiwa kukamatwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Wilaya ya Kahama (TAKUKURU) wakiwa na dawa za aina mbalimbali ikiwemo drip za maji kwenye pochi zao za mkononi (Handbag).


Mkurugenzi wa halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Anderson Msumba amekiri wauguzi hao kufikishwa kituo cha polisi Kahama kwa ajili ya kuhojiwa huku akisema kwa muda mrefu wamekuwa wakipokea malalamiko kutoka kwa wagonjwa kuwa wanauziwa dawa usiku wa manane.


Msumba amesema malalamiko ya wagonjwa waliendelea kuyafanyia kazi na TAKUKURU siku ya Februari 24, 2023 walishtukiza katika hospitali ya Wilaya na kufanya ukaguzi huo ambapo katika wauguzi wa zamu za usiku, saba walikutwa na dawa kwenye mikoba yao.


Aidha mkurugenzi huyo amesema kitendo kilichofanywa na watumishi hao ni kuikosesha mapato halmashauri sambamba na kuhatarisha afya za wagonjwa kwani usalama na ubora wa dawa hizo na zilikotoka hazijulikani.


Amesema uchunguzi wa Jeshi la polisi utakapokamilika na kupata ukweli na wao ndio watachukua hatua zingine za kiutumishi huku akiwataka watumishi kada ya afya kuacha tabia ya kuuza dawa usiku wa manane.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso