ANAYETUHUMIWA KUUA MKE WA MWENYEKITI WA MTAA WA NATIONAL HOUSING,RWAMISHENYE-BUKOBA,TAYARI YUKO MIKONONI MWA POLISI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 21 February 2023

ANAYETUHUMIWA KUUA MKE WA MWENYEKITI WA MTAA WA NATIONAL HOUSING,RWAMISHENYE-BUKOBA,TAYARI YUKO MIKONONI MWA POLISI





JESHI la polisi mkoani Kagera,linamshikilia Paschal Kaigwa Mariseli(21) kwa tuhuma ya mauaji ya Hadija Ismail(29),mkulima na mkazi wa National Housing kata na tarafa ya Rwamishenye katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera,tukio lililotokea Februari 13,2023.


Hadija alikuwa mke wa Mwenyekiti wa eneo hilo la National Housing.


Akiongea na vyombo vya habari Jumanne 21 Februari 2023,Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera,ACP William T.Mwampaghale,amesema kijana huyo baada ya kutekeleza mauaji hayo,alikimbilia vichakani alikojificha kwa muda wote huo hadi alipozidiwa na njaa na kuamua kutoka mafichoni na kwenda kuomba msaada wa chakula kwa shangazi yake aishiye mtaa wa Kashai,manispaa ya Bukoba.


Aliwakuta watoto wa shangazi yake waliokuwa wanamtambua,na kwa kuwa tukio hilo lilikuwa kimetangazwa sana na vyombo vya habari,walipiga kelele na majirani wakafika na kumkamata majira ya saa kumi jioni tarehe 19/02/2023.


Mtuhumiwa ambaye ni mzaliwa wa kijiji Katerero,Bukoba vijijini,alikuwa amepewa hisani na mwenyekiti wa eneo la National Housing,tangu mwezi Novemba 2022,wakiishi naye.


Jeshi la polisi limevishukuru vyombo vya habari na wananchi kwa ujumla kwa ushirikiano na kuomba waendelee kufichua vitendo vya kihalifu na pia wanachi wavumiliane kunapokuwa na migogoro na siyo kuchukua hatua za kuua.


Amewaonya wanachi kutojihusisha na vitendo vya kihalifu ikiwemo mauaji,ubakaji na ukatili mwingine,na kuwa hatua kali zitachukuliwa kwa watakaojihusisha na vitendo hivyo.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso