Watu wawili wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wenye umri kati ya miaka 25 hadi 30 wameuawa na Jeshi la Polisi mkoani Kagera na kisha kukutwa na bunduki moja aina ya AK 47, risasi 25 na mabomu mawili ya kurusha kwa mkono.
Watu hao wanaodhaniwa ni majambazi ambao bado hawajafahamika wameuawa Januari 21, 2023 na miili yao imehifadhiwa katika Hospitali ya Nyamiyaga wilayani Ngara kwa ajili ya kutambuliwa na kwa uchunguzi zaidi.
Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema kuwa, tukio limetokea Januari 21, 2023 saa 3:35 usiku katika maeneo ya Barabara ya Kumunazi kwenda Relenge, Wilaya ya Ngara.
“Jeshi letu lilipata taarifa ya siri kwamba kuna kikundi cha waharifu kimepanga kufanya uharifu kwa kutumia silaha katika katika maeneo ya Kumunazi siku ya Januari 21, 2023 usiku na watatumia usafiri wa pikipiki hivyo tuliandaa mtego katika barabara zote zinazoingia Kumunazi,” amesema.
“Ilipofika majira ya saa 21:35 usiku katika maeneo ya barabara ya Kumunazi kwenda Rulenge ilitokea pikipiki iliyokuwa imebeba watu watatu hivyo askari waliokuwa doria katika barabara hiyo walijaribu kuisimamisha lakini walikaidi na kugeuza kurudi walikotoka,” ameeleza.
No comments:
Post a Comment