Mhandisi Ayoub Mwenda akizungumza katika mkutano uliowakutanisha waathirika wa tope la mgodi wa Williumson Diamond pamoja na uongozi wa Halmashauri.
Wananchi walioathirika na tope lililotoka kwenye mgodi wa mwadui (Williumson Mwadui LTD) wakiwa kwenye mkutano huo.
NA HALIMA KHOYA-SHINYANGA
Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kijiji cha Mwangholo Halmashauri yaWilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga uliowakutanisha waathirika, uongozi wa mgodi na wawakilishi wa halmashauri wamesema kuwa suala hilo limechukua muda pasipo kutolewa majibu yanayoleta faraja kwao huku suala la wao kuhamia katika makazi mapya likiwa bado ni changamoto.
Akizungumza kwa niaba ya waathirika wa tope hilo kwenye mashamba,Ester Nguli,Amesema ulipwaji wa fidia kwa waathirika wa nyumba unatekelezwa kwa uharaka zaidi ukilinganisha na waathirika wa mashamba wanacheleweshwa kulipwa fidia zao huku wakisingizia kufanya tathmini kwa kina.
" Kwa watu walioathiriwa kwenye nyumba wamelipwa fidia kwa kupewa makazi na vyakula lakini sisi tulioathiriwa mashamba ambayo tunalima mazao ya chakula bado hatulipwi fidia,na mpaka sasa hivi hatujapatiwa mbadala wowote ule,tunaambiwa bado wanafanya tathmini,sasa hivi watu hatuna chakula tunakula mtama kila siku,Miezi ya kulima inaisha tutalima muda gani,tunauomba uongozi utusaidie kwakweli hali zetu ni mbaya"Amesema.
Nae muathirika wa tope kwenye makazi,Levocatus shijja,amesema hawatakubali kuhama katika makazi ya yakuzaliwa na kwenda katika kijiji cha ukenyenge kufuatia kikao cha madiwani kilichofanya uamuzi huo ambapo wameitaka serikali kuondoa tamko hilo na kuwasaidia kuondokana na changamoto zao.
"Kuna baadhi ya watu wanalipwa naa wengine hawalipi,kinachotia kichefuchefu zaidi ni uamuzi uliotolewa na madiwani katika kikao na kwamba wanataka waathirika wote wa tope wahamie ukenyenge sasa tunasema hivi hatuhami hata kwa bunduki"Amesema
Aidha kwa upande wake Muhandisi Ayoub Mwenda,ambaye ni meneja mkuu katika mgodi huo,amesema Fidia zote zitatolewa kwa waathirika hao pamoja na usumbufu uliojitokezaa kipindi chote huku akiwataka wananchi hao kuwa wavumilivu wakati wanafanya tathmini ya athari iliyojitokeza ili kuhakikisha kila mmoja anapata anachostahili.
"Fidia zote itajumuishwa pamoja na fidia ya usumbuhi hivyo tunawaomba wananchi muwe naa subra hivi karibuni tutalizaa kufanya tathmini ili kuhakikisha kila mmoja anapata anachostahili"Amesema.
No comments:
Post a Comment