Serikali imesema muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ukipitishwa na kuwa sheria na kuanza kutumika mwaka huu, mwananchi yoyote ambaye hatakuwa na bima hiyo kuanzia mwaka 2026, hataweza kupata huduma zingine ikiwamo leseni ya udereva.
Kauli hiyo imetolewa leo na mjumbe wa sekretatieti ya bima ya afya kwa wote kutoka Wizara ya Afya, Jackline Tarimo wakati akitoa mada kwenye kikao cha wadau wa afya mkoani Mwanza kilicholenga kufanya tathmini ya utoaji wa elimu kwa umma kuhusu umuhimu wa bima ya afya kwa wote.
Tarimo amesema ukifika muda huo watu wote wasiofanya kazi katika sekta rasmi, watakapokuwa wanahitaji huduma mbalimbali kutoka taasisi za umma watatakiwa kuonyesha kadi ya bima ya afya kwa wote.
“Ikifika mwaka 2026, mtu akienda kupata huduma muhimu sehemu kama vile kukata leseni ya udereva pamoja na wanafunzi wanaoanza vyuo vikuu, watatakiwa kuonyesha kadi ya bima ya afya,” amesema.
Amesema lengo la serikali kufanya hivyo siyo kuwatesa wananchi wake bali kufanya upatikanaji wa huduma ya afya kwa wote kuwa kipaumbele kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment