Papa Francis ameongoza mazishi ya aliyekuwa Papa Benedict siku ya Alhamisi, akigusa kwa upole jeneza la mtangulizi wake alipokuwa amesimama kwenye fimbo mbele ya makumi ya maelfu ya waombolezaji, huku wengine wakitaka marehemu papa afanywe mtakatifu.
Kifo cha Benedict siku ya Jumamosi kilihitimisha muongo mmoja wa papa huyo wa zamani na wa sasa akiishi bega kwa bega huko Vatican na ilikuwa ni mara ya kwanza katika kipindi cha zaidi ya miaka 200 kwamba papa mmoja aliongoza ibada kwa ajili ya mtangulizi wake.
Mapapa watatu kati ya watano wa mwisho wamefanywa kuwa watakatifu, lakini ni karibu theluthi moja tu ya mapapa wote wametangazwa kuwa watakatifu katika historia ya miaka 2,000 ya Kanisa.
Wakati viongozi wengi wakimsifu Benedict tangu kifo chake, ukosoaji pia umetangazwa, ikiwa ni pamoja na waathiriwa wa unyanyasaji wa kingono wa makasisi, ambao wamemshutumu kwa kutaka kulilinda Kanisa kwa gharama yoyote.
Francis, ambaye alikaa kwa muda mwingi wa ibada kwa sababu ya ugonjwa wa goti, aliinuka mwishoni wakati jeneza la Benedict likibebwa kwa maziko ya faragha ndani ya Kanisa Kuu la Mtakatifu Petro. Akiinamisha kichwa chake katika sala ya kimya, Francis aligusa sanduku kwa muda mfupi.
CHANZO: BBC
No comments:
Post a Comment