Milio ya risasi na milipuko mikali imesikika Jumanne asubuhi katika kambi ya kijeshi katika ya mji wa Hawadley katika eneo la Shabelle ya kati nchini Somalia.
Mamlaka zinaamini kuwa shambulizi hilo limetekelezwa na watu wanaoshukiwa kuwa wanachama wa kundi la wanajihadi la al-Shabab.
Afisa mkuu wa jeshi ni miongoni mwa waliouawa katika uvamizi huo lakini bado kuna taarifa kamili kuhusu idadi kamili ya waliouawa.
Tukio hili linakuja siku chache baada ya jeshi kuteka bandari ya kimkakati ya Haradhere ambayo imekuwa ikishikiliwa na kundi la kijihadi kwa miaka 15.
Al-Shabab wamepoteza maeneo mengi tangu Agosti mwaka jana, wakati wanajeshi wa serikali wakisaidiwa na wanamgambo wa koo walipoanzisha mashambulizi kusini na katikati mwa Somalia.
Lakini kundi hilo limeendelea kufanya mashambulizi dhidi ya majengo hasa ya serikali na wanajeshi wa Umoja wa Afrika.
Wiki iliyopita, ilifanya mashambulizi manne mabaya ya mabomu katika eneo la kati la Hiran.
CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment