Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha mbolea Itracom, Nduwimana Nazaire (katikati) akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari walipotembelea eneo la uzalishaji kueleza kazi inayofanywa na mitambo iliyopo eneo hilo.
Eneo la kuhifadhia mbolea kiwanda cha Itracom.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (TFRA), Dkt. Stephan Ngailo akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari walipotembelea kiwanda cha mbolea cha Itracom Nala Jijini Dodoma tarehe 11 Januari, 2023.
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania(TFRA),imesema hadi sasa imesajili aina 420 za mbolea zenye kukidhi viwango vinavyotakiwa nchini katika kuhakisha inakabiliana na uhaba wa mbolea,matarajio yakiwa ifikapo mwaka 2030 kusiwepo uagizaji wa mbolea toka nje.
Hii inakwenda sambamba na ujenzi wa viwanda vya mbolea kuhakikisha ifikapo mwaka 2025,uzalishaji wa mbolea nchini unafikia tani 800,000.
Hayo yamesemwa tarehe 11 Januari 2023 na Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania,Dr Stephan Ngailo wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo vya habari nchini,kutembelea kiwanda cha uzalishaji mbolea cha Itracom kilichoko eneo la Nala,Jijini Dodoma.
Kiwanda hicho cha Itracom kimejikita katika kuzalisha mbolea za asili (organic mineral fertilizer) zinazofanya vizuri kwenye uzalishaji na kimejengwa kwa muda wa mwaka mmoja na miezi mitano mpaka kilipoanza uzalishaji wa awali.
Kwa Upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Itracom, Nduwimana Nazaire amesema, awali mwekezaji alijipanga kuzalisha tani laki sita lakini kufuatia mahitaji makubwa ya mbolea nchini atazalisha tani milioni moja kwa mwaka.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa uongozi wa kiwanda hicho umejipanga kuhakikisha wanazalisha mbolea zenye ubora wa viwango vya juu na rafiki kwa udongo na mazingira ya eneo husika lengo likiwa ni kuongeza uzalishaji wa mazao mbalimbali nchini na hivyo kuwaongezea tija wakulima.
No comments:
Post a Comment