KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE KUANZA VIKAO WIKI IJAYO - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 5 January 2023

KAMATI ZA KUDUMU ZA BUNGE KUANZA VIKAO WIKI IJAYO

Vikao vya kamati za kudumu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania vinatarajia kuanza Januari 9, 2023 ambapo kamati mbili za Sheria Ndogo na Masuala ya Ukimwi zitakutana kuanza kupokea taarifa mbalimbali.


Taarifa iliyotolewa leo Januari 5, 2022 na Ofisi ya Bunge, imebainisha kwamba vikao hivyo kwa kamati zote za Bunge vitaanza Januari 16, 2023 jiji Dodoma ambavyo ni maandalizi ya mkutano wa 10 wa Bunge.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Bunge, kamati zitapokea na kujadili mambo sita ikiwemo taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge yaliyotolewa taarifa ya mwaka katika shughuli za kamati zilizowasilishwa Februari 2022.



Vilevile, watapokea taarifa zinazohusu shughuli za umma nchini ili kufuatilia utekelezaji wa sera na mipango ya sekta zinazohusika na kupokea na kuchambua taarifa za uwekezaji wa mitaji ya umma ili kubaini kama uwekezaji huo una ufanisi na umezingatia sheria.


“Kuchambua taarifa za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kuhusu ukaguzi maalumu na kaguzi za ufanisi, shughuli hii imepangwa kwa kamati mbili za kudumu za Bunge ambazo zinasimamia matumizi ya umma,” inasomeka sehemu ya taarifa ya Bunge.


Taarifa ya ukusanyaji wa mapato pia itapokelewa na kujadiliwa ambapo huenda moshi wake ukafika ndani ya vikao vya bunge hasa kutokana na kelele nyingi kwa wananchi kuhusu vibano kwenye suala zima la kodi ambapo vyanzo vya mapato na utekelezaji wa bajeti vitajadiliwa pia.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso