ZAIDI YA MIL.144 ZATOLEWA NA MANISPAA KWAAJILI YA VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU,RTO SHINYANGA AONYA MISHIKAKI KWA BODABODA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 2 December 2022

ZAIDI YA MIL.144 ZATOLEWA NA MANISPAA KWAAJILI YA VIJANA NA WATU WENYE ULEMAVU,RTO SHINYANGA AONYA MISHIKAKI KWA BODABODA

Baadhi ya bodaboda Mkoani Shinyanga,wameaswa kufuata sheria za barabarani kwa kufuata alama na kiwango cha kupakia abiria katika pikipiki zao ili kuondokana na adha ya kuwepo kwa ajali zisizotarajiwa ambazo zinasababisha kuwepo kwa uharibifu wa mali za umma na vifo kwa watu wasio na hatia.

Mkuu wa Mkoa shinyanga,Sophia Mjema wakati wakikabidhiwa Bodaboda zao


NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA

Akizungumza katika zoezi la kukaidhi pikipiki 34 na bajaji 3, Afisa usalama barabarani Mkoani humo(RTO),Debora Lukololo,ambapo zoezi hilo lilifanyika katika stendi mpya ya haice Kambarage katika Manispaa na Mkoa Shinyanga.


Debora,amesema kumekuwa na idadi kuwa ya ajali zinazosababishwa na uendeshaji mbaya sambamba na kupakia abiria Zaidi ya kiwango (Mishikaki) ambapo amewataka vijana hao waliopewa pikipiki 34 na bajaji 3 ikiwa na thamani ya Mil.144 424,000/= Tsh kwaajili ya kuwapatia ajira ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.


Aidha Debora amesema kuwa kumekuwa na waendesha pikipiki wanaopakia bidhaa ambazo zinahatarisha usalama kwake na watumiaji wengine wa barabara (Mbao ndefu,nondo,mabati),sambamba na kutokuwepo na vioo angalizi(Site mirror)kwenye pikipiki zao,ambapo amesema hataki kuona aina hiyo ya usafirishaji na kuwataka wawaachie madereva wa magari kupakia bidhaa hizo ili kuepusha ajali.


“Ajali nyingi sasa ivi ni za bodaboda,mnapakia abiria wengi(Mishikaki),mnaendesha mwendo mbaya,hamtii taa za barabarani ,mnabeba bidhaa ndefu kiasi kwamba mnafunga barabara,nikikukamata pikipiki yako itaozea kituoni,niwatake mkawe watiifu kwenye usafirishaji wenu wa abiria”Amesema Debora.


Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga,John Tesha,ameeleza vikundi vilivyopatiwa mkopo na halmashauri hiyo imetoa mikopo kwa vikundi tisa(9)(kikundi cha USA peoples disability(Mil.9),Malida peoples disability (Mil.18), kikundi cha hisa mageuzi (mil.3), kikundi cha princes( Mil.10),kikundi cha ushonaji B(mil.13),nguvu kazi cha vijana(mil.26),kikundi cha waendesha boda boda (mil.26),kikundi cha bodaboda Nshola Mwamalili (mil.26) na kikundi cha uwezesha).


Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya Shinyanga,Jasinta Moneko,Amewataka wananchi waendelee kujiunga katika vikundi mbalimbali ili kujenga ushirikiano baina yako hatimae kuweza kuunda kikundi kwaajili kuchukua mikopo katika halmashauri zao ili kuondokana na vijana wasiokuwa na ajira katika jamii.


Aidha kwa upande wake Mkuu wa Mkoa shinyanga,Sophia Mjema,ameipongeza halmashauri kwa hatua kubwa waliyopiga aambamba na kuamua kuleta mfumo mzuri wa kutoa bidhaa na siyo fedha taslim kwa wananchi ili kuondokana na adha ya ucheleweshaji wa marejesho ya mikopo hiyo.


Nao baadhi ya vijana na walemavu waliopewa mikopo hiyo wameishukuru Halmashauri kwa kuwaamini na kuweza kuwanunulia vifaa hivyo vya usafirishaji na mikopo hiyo kwaajili ya kuanzisha biashara mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo.

Mkuu wa Mkoa shinyanga,Sophia Mjema akikabidhi mfano wa hundi ya mkopo 

Afisa usalama barabarani Mkoani humo(RTO), Debora Lukololo akizungumza na umati uliofika katika zoezi la utoaji wa mikopo hasa vijana waliopata vyombo vya moto Bajaji na Pikipiki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso