UMKI WASEMA NGUVU ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA KUUONDOA MKOA WA KAGERA KWENYE LINDI LA UMASKINI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 30 December 2022

UMKI WASEMA NGUVU ZA PAMOJA ZINAHITAJIKA KUUONDOA MKOA WA KAGERA KWENYE LINDI LA UMASKINI

Mbunge wa Jimbo la Nkenge, Florent Kyombo (mwenye suti nyeusi katikati), kulia kwake ni Mwenyekiti wa UMKI, mhandisi Godfrey Mugini, na kushoto kwake ni Magreth Mugyabusò, Katibu mtdndaji UMKI wakiwa na walimu baada ya kuwakabidhi vitabu




UMOJA wa maendeleo wa kijiji cha Kikukwe(UMKI),katika kata ya Kanyigo,wilaya ya Missenyi,umesema lengo lao ni kuendelea na kupambana na umaskini hadi kijiji hicho kufikia kiwango cha juu cha maendeleo.


NA MUTAYOBA ARBOGAST,BUKOBA


Awali mh mbunge wa Jimbo la Nkenge,Florent Kyombo,kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Missenyi, Desemba 27,2022,amekabidhi vitabu vya kiada ba ziada vyenye thamani ya sh milioni 11.5 kwa walimu wakuu na wakuu wa shule,vilivyotolewa na UMKI kwa shule zote kumi za msingi na nne za sekondari,za serikali na binafsi ili kuongeza kiwango cha ufaulu,huku akiwasisitiza walimu na wanafunzi kuvitunza.


Wakiwa katika maadhimisho ya mwaka wa pili tangu kuundwa kwa umoja huo ambao tayari umesajiliwa katika Halmashauri ya wilaya ya Missenyi,Mwenyekiti wa UMKI,mhandisi Godfrey Mugini,amesema wakati wa sherehe ya Kikukwe Day kuwa tatizo la umaskini linaanzia na mtu binafsi mwenyewe,familia,kijiji,kata tarafawilaya na mkoa,kutokana na watu kutojibidiisha kufanya kazi.


Katika kukabiliana na umaskini ,kijijini,UMKI,iliyoasisiwa na wazawa wa kijiji Kikukwe waishio nje katika mikoa mbalimbali,waliamua kurudisha fadhila nyumbani kwa kupanga mipango ya maendeleo na kuwashirikisha wenyeji kijijini,katjka sekta za uchumi,elimu na afya.


Ameonesha matumaini yake kuwa kiwango cha utekelezaji wa mipango waliyoainisha, ikiwa ni pamoja na kilimo cha Avocado aina ya Has unatia moyo,na hivyo utachochea vijiji jirani hadi kusambaa hadi mkoa mzima.


"Umaskini mwingine ni wa kujitakia.Hebu angalia baadhi ya vijana wetu,tangu asubuhi ni kulewa tu,sasa hapo umaskini unaondokaje?"amehoji Mugini,huku akiongeza kuwa,tayari uongozi umewasiliana na Afisa mtendaji wa kata ili suala la kutofanya kazi na kuendekeza ulevi,vinatafutiwa 'muarobaini'.


Mugini ameeleza pia azma yao kuifanya senta ya Omurushenye kuwa ya kibiashara zaidi ili kuchochea uchumi.


Mwenyekiti wa kijiji hicho Josephat Ikulla,amesema siri ya mafanikio ni ushirikishwaji,na wananchi kujitambua kwani wenyeji walikubaliana kuchangia sh 21,000 kwa mwaka,huku waishio nje wakirudisha fadhila,hadi kufikia hali inayotia matumaini.


Magreth Mugyabuso ambaye ni Katibu mtendaji wa UMKI,amesema umoja huo wamefanikiwa kujenga msingi na ambao tayari umetandazwa jamvi,jumla ya gharama za ujenzi sa msingi huo,ni zaidi ya sh milioni 35,huku kwa mwaka 2023 wakitarajia kumaliza ujenzi huo wa Hosteli ya wasichana shule ya sekondari Kikukwe,ambapo mwananchi wa kijijini atachangia sh 35,000 mwaka 2023.


Katika harambee ya uchangiaji ujenzi wa hosteli hiyo,fedha taslimu pamoja na ahadì,ilipatikana zaidi ya sh milioni 15.





No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso