Stand ya haice kambarage ikiendelea na ujenzi.
Bodaboda anayefanya kazi pembezoni mwa Stand mpya inayojengwa Kambarage,Juma Mussa
Mfanyabiashara aliyepembezoni mwa stand mpya ya haice iliyokatika ujenzi kabarage,paul Masaba
Baadhi ya wafà nyabiashara na waendesha pikipiki maarufu kama bodaboda, Manispaa ya Shinyanga, wameipongeza manispaa Kwa kuboresha miundombinu mbalimbali pamoja na stand ya haice iliyopo Kambarage, itakayowasaidia kuongeza kipato na uzalishaji katika kazi zao.
NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA
Hayo yamebainishwa hivi karibuni na wafanyabiashara pamoja na waendesha bodaboda Mkoani humo wanaofanya kazi jirani na stand mpya ya haice kambarage ambayo itakamilika hivi karibuni.
Wafanyabiashara hao wameeleza mchango utakao patikana baada ya kukamilika kwa stand hiyo ambapo itapelekea kuongezeka kwa watu kutoka sehemu mbalimbali huku wakiipongeza Manispaa ya Shinyanga kwa kuboresha miundombinu rafiki kwa Wananchi.
Kwa upande wake mwendesha pikipiki (bodaboda),Said Hamis,Amesema stand hiyo itawasaidia kuongeza uzalishaji na upatikanaji wa abiria hali itakayosaidia kuondokana na adha la kupaki muda mrefu.
Aidha kwa upande wao Wafanyabiashara wanaoizunguka stend hiyo wamebainisha kuwepo kwa dosari kubwa waliyoipata baada ya kuhamishwa kwa soko la mbao hali iliyopelekea kuwepo na mzunguko mdogo wa bidhaa za ujenzi katika maduka yao.
Akizungumza kwa niaba ya wanawake walionania ya kujikwamua kiuchumi na kujikita kwenye biashara,Bi Petti, ambapo ameiomba Manispaa kutoa mikopo kwa mtu mmoja mmoja ili kuondokana na adha ya kulipishwa madeni makubwa yanayosababishwa na kutoroka kwa mmoja wa kikundi watakaochukua mkopo.
"Ujenzi wa Stand ya haice kambarage kutasaidia kuongezeka kwa wateja kutoka sehemu tofauti tofauti kutokana na mwingiliano mkubwa utakaopelekea kuleta maendeleo na kuongeza mzunguko mkubwa wa biashara,licha ya kuwepo kwa dosari kubwa tuliyoipata baada ya kuondolewa kwa soko la Mbao lakini tunaishukuru Manispaa kwa kutuletea stend hii"Amesema Petti.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga,Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,John Tesha,Amesema Manispaa imelenga kujenga na kuboresha miundombinu mbalimbali huku akibainisha kuwa mikopo ya Manispaa inatolewa kwa vikundi na siyo kwa mtu mmoja mmoja ambapo imelenga kutolewa kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu ikiwa ni sheria kwa nchi nzima.
"Mikopo inayotolewa na Manispaa hutolewa kwa vikundi tofauti tofauti (Wanawake,vijana na watu wenye ulemavu),hivyo mikopo inayotolewa kwa mtu mmoja mmoja inatolewa na taasisi za kifedha ambapo ni mikopo yenye riba hivyo mikopo ya Manispaa haina riba,Kufikia 2025 Manispaa imejipanga vyema kuboresha maeneo mbali mbali,(Soko la Lubaga,soko la Kambarage,Lori Paking na Maduka makubwa),Ili kuweka mazingira rafiki katika jamii"Amesema Tesha.
No comments:
Post a Comment