MKUTANO Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Kata za Kanyigo na Kashenye (Kanyigo and Kashenye Development Association-KADEA), wilayani Missenyi,kwa mara nyingine limewachagua Enock Kamuzora (Mwenyekiti),Godfrey Kamukala(Katibu mkuu),na Mwesiga Kahwa (Mwekahazina)ambaye amegombea nafasi hiyo kwa mara ya kwanza kuongoza umoja huo kwa kipindi cha miaka mitatu.
Meza Kuu katika Mkutano Mkuu kadea
Na Mutayoba Arbogast, Huheso Digital Bukoba
Mkutano huo umefanyika ukumbi wa shule ya sekondari Kanyigo,20 Desemba 2022,na umehudhuriwa na wajumbe 320.
Aidha mkutano huo,umewachagua pia viongozi wengine akiwamo Mary Kassano,ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uongozi,uchaguzi uliosimamiwa na Mjumbe wa Bodi,Emmanuel Makubo.
Umoja huo unamiliki shule ya sekondari Kanyigo yenye kidato cha kwanza hadi cha sita;na pia mradi wa Kituo cha mafuta.
Enock Kamuzora amewaeleza wajumbe mkutano mkuu kuwa wanaendelea kusimamia maadili ya wanafunzi na walimu,kuinua kiwango cha wanafunzi bila kujiingiza kwenye vitendo vya udanganyifu katika mitihani,ili kushinda kwa haki na si vinginevyo.
"Mtoto anayepita kwa udanganyifu hawezi kufanya vizuri ngazi za juu.Elimu yenye udanganyifu si elimu bali ujinga wa hali ya juu",amesema Kamuzora.
Ametaja baadhi ya mafanikio ya shule hiyo ya Sekondari Kanyigo,kuwa kwa mwaka 2021,matokeo ya mitihani kitaifaKidato cha nne walipata daraja la kwanza 64, daraja la pili 73,la tatu 16 na la nne 0.
Kwa Kidato cha sita mwaka 2022,daraja la kwanza ni 12,la pili ni 17,la tatu 7 na la nne 0.
Changamoto wanazokumbana nazo hasa zinatokana na wanafunzi wengi wanaomaliza darasa la saba karibu wote kujiunga na shule za serikali kwani mapato ya mwananchi mmoja mmoja yamepomoka kutokana na kuyumba kwa uchumi.
Aidha katika kukabiliana na upungufu wa kipato imeazimiwa kuwa kila mwanachama awe na miche 100,ambayo pia ni lazima kwa mwanachama mpya anajiunga na KADEA.
Mwanachama Chrisant Mujambula,amewahimiza wanachama na jamii kwa ujumla kuitangaza KADEA kifua mbelekutojana na mafanikio yake badala ya kuongea oembeni na kuisimanga kama wanavyofanya baadhi ya watu.
No comments:
Post a Comment