MAELFU YA WATU WAMEHUDHURIA KWENYE MAZISHI YA RICHARD NZUMBI,MAMA MZAZI WA RICHARD ASEMA HAYA,SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 23 December 2022

MAELFU YA WATU WAMEHUDHURIA KWENYE MAZISHI YA RICHARD NZUMBI,MAMA MZAZI WA RICHARD ASEMA HAYA,SHINYANGA

Watu wakiwa malaloni,wakiendelea na zoezi la kumzika Richard Nzumbe.


Majonzi na Simanzi vikiwa vimetawala mahali hapa katika zoezi la kuuaga na kwenda kuuhifadhi mwili wa Richard Nzumbi aliyefariki baada ya shambulio la risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi ambapo alisema wakati wanuhai wake, akifariki basi akazikiwe nyumbani kwao.


NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA


Zoezi hilo la kuuaga na kwenda kuuhifadhi mwili,Richard Nzumbi limefanyika jana Desemba 22,Mwaka huu,Kata ya Mega Kijiji cha Masaabi Halmashauri ya Wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga.


Akieleza historia ya marehemu, amesema Richard Nzumbe alizaliwa 1/1/1988 Katika kijiji cha Masaabi ambapo alianza shule ya msingi 2000 katika shule ya msingi Msingu na kumaliza sekondari 2010 kisha kujiunga na chuo cha ufundi veta shinyanga,Alioa 2013 ambaye hadi kufikia umauti wake Desemba 20 akiwa ameacha watoto watatu(Wote wakike) na mke wake akiwa na mimba.

"Tarehe 1,8,1988 Alizaliwa Richald Nzumbe,makaa 2000 alianza shule ya msingi Msingu,2010 alimaliza sekondari kwenye shule ya sekondari Baloha na kuoa 2012,marehemu alianza kufanya kazi akiwa mlinzi katika Kampuni ya SGA akiwa na chumba chake anachofanyia kazi ya wakala wa m-pesa kufikia 20,desemba mwaka huu marehemu alivamiwa na watu wasiojulikana wakampiga na risasi 8,majirani walimpeleka hospitali ya rufaa,saa 10 alfajiri aliaga dunia"Amesema.


Kwa upande wake Mama mzazi wa Richald Nzumbe,Ester Muhekela,amesema kuondoka kwa mwanae kumemuumiza sana hukua akieleza kuwa alikuwa akimtegemea Richald kwa sababu huyo ndiye mtoto wake wa kwanza ambapo alimuahidi kumjengea nyumba.


Awali,Ester Muhekela,Amebainisha kuwa amekwisha achika na mume wake baada ya kupigwa na mume wake hali iliyopelekea kuvunjika mkono.


"Richald ni mtoto wangu wa kwanza nilimsomesha mwenyewe,nilikuwa nauza vyungu ili kulipa ada ya mwanangu,mume wangu alikuwa ananipiga sana hadi akanivunja mkono,Richald aliniahidi kunijengea nyumba hivyo sina tegemeo jingine tena"Amesema Muhekela.


Nae Mwenyekiti wa mtaa huo, Hassani Mayala,amesema msiba huo wameupokea kwa majonzi sambamba na kulaani waliohusika na mauaji ya Richard kwa kuwa ni kitendo cha kikatili.


Akizungumza kwa niaba ya Mawakala wa Fedha,Danford Masawe,amesema msiba huo umewagusa na kuwaachia majonzi makubwa huku akiiomba serikali kuwawekea ulinzi shirikishi kulingana na biashara zao kuwa hatarishi na kuliomba jeshi la polisi kutofumbia macho tukio hilo sambamba na kutoa adhabu kali kwa watakaobainika kuhusika na kifo cha Richald ili kuwa funzo kwa wengine majambazi wa aina hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso