KISA KULIMA NA KUCHUNGA NG'OMBE WANAFUNZI HAWAENDI SHULE,SHINYANGA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Friday, 9 December 2022

KISA KULIMA NA KUCHUNGA NG'OMBE WANAFUNZI HAWAENDI SHULE,SHINYANGA.

Zikiwa zimebaki siku 3 za kutamatisha siku 16 za kupinga ukatili Mkoani Shinyanga ,baadhi ya wanafunzi wa Shule ya msingi Nyida iliyopo Mkoani humo wameiomba serikali kuwachukulia hatua wazazi wanaowakataza watoto wasiende shule badala yake wanawapeleka kulima na kuchunga ng'ombe hali inayowadumaza watoto hao kwenye sekta ya elimu.



NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA.

Wakizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni wanafunzi hao wameeleza namna wanavyoumizwa na vitendo hivyo ambapo wanaiomba serikali uweza kuwachukulia hatua wazazi hao.


Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi,Godfrey Mwankalage,amesema wamekua wakiwaona baadhi ya wanafunzi wenzake hawaji shule na sababu ikiwa ni kuzuiwa na wazazi wao ili wakalime na kuchunga mifugo yao.


Kwa upande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi Shule ya msingi Nyinda,Julias Mwakalebela,Amesema watoto hao wanachangamoto kubwa katika utafutaji wa elimu kwa kupewa kazi za kulima na kuchunga mifugo baada ya kuhudhuria mashuleni hali inayopelekea kuongezeka kwa idadi ya watoro katika shule hiyo.


"Watoto wakiwa wanakuja shule mara wanaambiwa waende shambani na kuchunga ng'ombe pia,hivyo sisi walimu tunakosa ni jinsi gani tutamsaidia maanafunzi huyu kwani hata tukimuita shule haji,tuaomba serikali iangalie hili kwa ukaribu ili kuwaweka watoto hawa salama"Amesema Mwakalembela.


Nae mwalimu Mlezi katika shule hiyo, Bi.Fabiola kolneli,amesema kumekuwa na ushirikiano mdogo kati ya wazazi na walimu, wanafunzi na wazazi hali ambayo inapelekea maendeleo hafifu ya mtoto awapo shuleni,huku akiiomba serikali.kutoyafumbia macho maovu wanayofanyia watoro hao.


Aidha kwa upande wake Afisa Elimu Kata ya Nyida,Martin Kingu Amethibitisha kuwepo kwa tatizo hilo kwa baadhi wanafunzi katika shule hiyo ambapo amesema kufikia muda huu imebaki asilimia chache ya wanafunzi wanao toroka shuleni hapo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso