KIKUNDI CHA JUHUDI CHATOA MSAADA WA BIMA YA AFYA KWA WAZEE WASIOJIWEZA KOLANDOTO - SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Monday, 5 December 2022

KIKUNDI CHA JUHUDI CHATOA MSAADA WA BIMA YA AFYA KWA WAZEE WASIOJIWEZA KOLANDOTO - SHINYANGA

kikundi cha hisa na maendeleo Juhudi kilichopo kata ya Ndembezi Manispaa ya Shinyanga kimetoa msaada wa baadhi ya mahitaji yao ikiwemo Bima ya matibabu kwa mwaka mzima itakayoisha 2024 kwenye kituo cha kulelea wazee Kolandoto.

Kikundi cha juhudi kikiwa pamoja na wazee wasiojiweza katika kituo cha kolandoto.


NA HALIMA KHOYA,SHINYANGA.


Akizungumza katika zoezi la kukabidhi msaada huo lililofanyika katika makazi ya wazee hao,Desemba 4,mwaka huu katika Kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga Mkoani humo,Afisa ustawi wa jamii Kata ya Ndembezi Jackson Njau Amesema.


Kikundi hicho kimefanya muendelezo wa kutoa msaada kwenye makundi ya watu wenye mahitaji maalum ambapo awamu hii wametoa msaada huo kwenye kituo cha kulelea wazee Kolandoto,na baadhi ya bidhaa walizozitoa ni pamoja na Bima ya afya itakayowasaidia wazee hao kujipatia huduma za afya kwa wepesi na pasina gharama yeyote.


Aidha Njau ameongeza kuwa katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake,wazee na watoto kikundi hicho kimeendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya athari za ukatili katika jamii ili kuondokana na vitendo vya ukatili.


"Kikundi hichi ni cha hisa na maendeleo ambapo wanakikundi hichi hutenga fedha kwenye mfuko maalumu kwaajili ya kutoa msaaada kwa watu wenye mahitaji maalumu,kikundi kimefanikiwa kutoa bidhaa kama Sukari,unga wa ngano,sabuni,dawa ya mswaki,vitunguu na sabuni ya kusafishia vyoo,utaendelea kutoa msaada huu kwa kila mwaka"Amesema Njau.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kikundi cha Juhudi,Sikujua Kitumbo ndani ya hisa kuna fedha kwaajili ya jamii na vikundi vingi haviwezi kuweka fedha hii kwaajioi ya watu wenye mahitaji maalum hivyo nakipongeza kikundi hichi tumeouga hatua kubwa,na kwa kipindi hichi cha siku 16 za kupinga ukatili kikundi chetu hatujakaa mbali tupo pamoja na jamii kwaajili ya kuwapatia elimu ya ukatili.


Aidha kwa upande wake Msimamizi wa kituo cha kulelea wazee Kolandoto ambaye kitaaluma ni afisa ustawi wa jamii,Amesema Jumla ya wazee waliopo katika kituo hicho ni 12 (Wakiume 11 na wakike 5 huku akieleza kuwa msaada huo utawasaidia kwa kipindi kigumu walicho nacho huku akifafanua manufaa watakayoyapata kwa kukatiwa bima hizo ambapo zitawasaidia kupunguza gharama za malipo ya kifedha sambamba na kuwarahisishia kupatiwa huduma za matibabu.


Nao baadhi ya wazee hao wamekishukuru kikundi cha juhudi kwa kuwaletea msaada huo ambapo wameeleza chagamoto walizokuwa wakikumbana nao wanapoenda hospitali kwaajili ya huduma za kiafya kipindi ambacho hawakuwa na bima,na kubainisha kuwa bima hizi zitawaondolea adha hizo.

Mlezi wa wazee wasiojiweza katika kituo kilichopo kolandoto,sophia kang'ombe akitoa shukrani kwa wanakikundi cha juhudi kwa msaada walioletewa.

Wanakikundi cha juhudi wakikabidhi bidhaa walizowapelekea wazee hao

Mwenyekiti wa kikundi cha juhudi,sikujua kitumbo akikabidhi bima kwa mlezi wa wazee hao



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso