Watumishi katika Halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera, wametakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya utumishi wa umma na kuzingatia nidhamu kazini, ili kujijengea heshima kwa jamii wanayoiongoza.
Mkuu wa wilaya ya Missenyi Kanali Wilson Sakulo
Hayo yamesema Mkuu wa wilaya hiyo Kanali Wilson Sakulo, na kusisitiza kuwa nidhamu ni muhimu katika uwajibikaji.
"Kwa mfano mwalimu sehemu aliyopo ni kioo kwa wale wanafunzi anaowafundisha, haileti afya kuona huyo mwalimu ndiye anakuwa mstari wa mbele kuangalia zile sketi zilizoko pale shuleni, nimeona kuna changamoto za namna hiyo zimekuwa zikitokea, mfano kuna mwalimu hapa amempa mimba mwanafunzi na amekimbia" amesema Kanali Sakulo.
Baadhi ya watumishi walioshiriki mafunzo hayo yanayolenga kuimarisha utendaji wao wa kazi, wamesema kuwa yatawasaidia katika utekelezaji wa majukumu hasa kwa watumishi wanaotoka vyuoni ambao hawajawa na uzoefu.
CHANZO:EATV
No comments:
Post a Comment