MKUTANO Mkuu maalum wa Chama cha waandishi wa habari mkoani Kagera(KPC),ambao umefanyika hotel ya ELCT manispaa ya Bukoba tarehe 21 Desemba 2022,umepitisha kwa kauli moja mapendekezo kadhaa yaliyoletwa mbele yake na Kamati tendaji,yenye lengo la kuboresha hali ya utendaji kazi kutoka mafanikio waliyonayo sasa hadi kuwa bora zaidi.
Mwenyekiti wa KPC,Mbeki Mbeki, Akifungua Mkutano Maalum wa Wanachama wa KPC katika Ukumbi wa ELCT katika Manispaa ya Bukoba.
Mwenyekiti wa KPC,Mbeki Mbeki, akiongoza Mkutano maalum wa wanachama wa KPC uliofanyika ukumbi wa ELCT Bukoba.
Na Mutayoba Arbogast, Huheso Digital Bukoba
Akifungua mkutano huo,,amesema Muungano wa vilabu vya habari Tanzania(UTPC) unafanya mabadiliko makubwa katika kuvijengea uwezo vilabu vya habari nchini kuwa na mikakati ya kujiimarisha na kujiendeleza,ili hata wafadhili wanaposuasua kutoa ruzuku au kujiondoa,vilabu viwe na uwezo wa kujiendesha bila kuyumba.
Katika kutimiza azma hiyo,pamoja na mambo mengine imedhamiria kuimarisha safu ya uongozi kwa kuunda Kamati ndogo ndogo chini ya Kamati tendaji.
Kamati hizo ni Kamati ya miradi,Kamati ya Maadili na Kamati ya huduma za jamii.
Aidha KPC inatarajia kuongeza wanachama kutoka 61 hadi 100,huku ikisisitizwa na wajumbe kuwa usajili wa wanachama usiwe katika mtindo wa 'zoazoa' bali wachujwe ili kukidhi viwango vya kitaaluma na kimaadili.
Kamati tendaji imekasimishwa madaraka na mkutano mkuu,kuingiza wanachama wapya,huku suala la ulipaji ada ya kila mwaka,ambayo ndiyo mapato msingi,likisisitizwa na kuwa ifikapo tarehe 31 Januari 2023,atakayekuwa na deni,atafukuzwa uanachama na hii ni kwa mujibu wa Katiba,na kuwa hakutakuwa tena na kuoneana haya katika kutimiza takwa hilo la kikatiba.
Katika hatua nyingine ya kujiimarisha toka kwenye bara na kuwa bora zaidi,KPC ipo kwenye hatua ya kutafuta jengo la ofisi lenye hadhi,mazingira nadhifu na yenye usalama na lenye kufikika kirahisi.
Katika uanzishwaji mradi wa uzalishaji ili kuiingizia fedha KPC,miradi kadhaa imependekezwa,na kuwekwa chini ya Kamati ya miradi kwa uchambuzi na hatua za utekelezaji.
Mkutano huo mkuu maalum,umeungana kwa njia ya simu na Mkurugenzi mtendaji wa UTPC,Kenneth Simbaya,ambaye pamoja na salaam za mkutano huo,ameahidi yeye,na Rais wa UTPC,Deogratias Nsokolo,kuwatembelea mwakani katika kujionea shughuli za maendeleo katika tasnia ya habari,na pia kuwatia shime.
Viongozi na wanachama wa KPC wakiwa katika mkutano katika ukumbi wa ELCT mjini Bukoba
No comments:
Post a Comment