Mwanamke Mmoja (35),Mkazi wa Iponya,Mariam Fransic, Ameuawa kwa kukatwa na panga kichwani na mume wake,Hamis Paulo (45),Mkazi wa Iponya, kisha na yeye kujinyonga na kamba hali iliyopelekea vifo vyao.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi
NA HALIMA KHOYA, Huheso Digital SHINYANGA.
Akieleza Juu ya tukio hilo la mauaji lililotokea Desemba 11 Mwaka huu majira ya saa 1 usiku, Mwenyekiti wa kitongoji cha Iponya Kata ya Kagongwa Halmashauri ya Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga Joint Willium Amesema.
Joint Willium, Amesema majira ya 1 usiku alipewa taarifa na baadhi ya wananchi wanaoishi jirani nyumba hiyo wakisema kuwa wanatia mashaka kuwepo kwa tatizo baada ya wakazi waliokuwa wakiishi ndani ya nyumba hiyo kutokuonekana kwa muda mrefu.
Willium amebainisha kuwa baada ya kufika katika nyumba hiyo walikuta mlango ukiwa umefungwa kwa ndani hali iliyosababisha kuvunja mlango ili kujua na kuona kilichopo ndani yake,ambapo baada ya kuvunja mlango huo walikuta mwili wa mwanamke huyo ukiwa umetapakaa damu na huku mwili wa mwanaume ukiwa unaning'inia juu na wote wakiwa wamekwisha kupoteza maisha.
Aidha Mwenyekiti Willium,Amesema kuwa tukio hilo ni lakusikitisha na lakikatili,ambapo mwanaume huyo inasemekana hakua mwenyeji katika kaya hiyo,awali mwanamke huyo alikuwa anaishi yeye na binti yake,ndipo walipomkaribisha mwanaume huyo katika makazi yao.
Willium amewaasa wananchi kutojichukulia sheria mkononi na kuwataka wawe wanafika katika mamlaka husika ili kuweza kutatua changamoto zao na kushikamana na elimu iliyotolewa katika kipindi cha siku 16 za kupinga ukatili kwa wanawake,watoto na watu wenye ulemavu ili kuondokana na vitendo hivyo.
"Majira ya saa 1 nilipewa taarifa kutoka kwa majirani,wenyeji wao hawaonekani katika nyumba,nilipofika tulivunja mlango tukakuta mwanamke umeuliwa kwa kukatwa panga kichwani na mume wake,na mwanaume alikuwa amejinyonga,huyu bwana alikuwa amekaribishwa kwa muda mfupi sana amekuwa na mwanamke huyo,hawajafunga ndoa wala hawana mtoto,Natoa wito kwa wakazi wa kitongoji changu wawe wanatoa taarifa pale wanapobainisha kuwepo kwa matukio ysiyoeleweka"Amesema Willium.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Shinyanga,ACP,Janeth Magomi,Amesema jeshi la polisi limegundua chanzo cha mauaji hayo inasadikika ni wivu wa mapenzi uliokuwa kati yao huku akibainisha kuwa dawati la Jinsia Mkoa Shinyanga litaendeleza kutoa elimi kwa wananchi licha ya kumaliza kuhitimisha kilele cha siku 16 za kupinga ukatili.
No comments:
Post a Comment