WAUAWA KWA KUPIGWA MAWE NA WANANCHI WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI,SHINYANGA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 9 November 2022

WAUAWA KWA KUPIGWA MAWE NA WANANCHI WALIOJICHUKULIA SHERIA MKONONI,SHINYANGA


Vijana wawili wakazi wa Mwanza, Saidi Ismail (29) na Paschal(20-25)wameuawa na wananchi waliojichukulia sheria Mkononi kwa tuhuma za kuvunja nyumba na kuiba katika nyumba ya Peter Mathias wakitaka kujipatia mali kwa njia iliyopelekea kifo chao.

NA HALIMA KHOYA, HUHESO Digital - SHINYANGA




Mauaji hayo yametokea Novemba 7,2022 majira ya saa 8 mchana katika kitongoji cha Butulwa Kata ya Old Shinyanga Wilaya na Mkoa Shinyanga.


Akizungumza kwa njia ya simu Mwenyekiti wa Kijiji Cha Old Shinyanga,Dotto Bwile amesema Tukio Hilo la mauaji limefanyika November 07 mwaka huu ambapo watuhumiwa wameuwawa baada ya kupigwa na wananchi sehemu mbalimbali za miili yao wakituhimiwa kuvunja nyumba ya Peter Mathias Mkazi wa Old Shinyanga na kuiba vitu mbalimbali katika nyumba hiyo.

Kwa upande wake Mganga Mfawidhi wa Hospitari ya Rufaa Mkoa wa Shinyanga John Ruzira amekiri kupokea Miili ya marehemu hao na kusema kuwa na mpaka Sasa miili hiyo bado imehifadhiwa katika vyumba vya kuhifadhia maiti.


"Jana nilipokea miili ya vijana wawili (Saidi Ismail (29) na Paschal(20-25 wakiwa wamekwisha kupoteza maisha ambapo hadi sasa hivi miili hiyo haijaja kuchukuliwa na ndugu wa vijana hao,hivyo ipo katika chumba cha kuhifadhia maiti"Amesema Ruzila.


Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga,ACP Janeth Magomi amekiri kupokea taarifa za tukio hilo huku akiwataka wananchi kutojichukulia Sheria Mkononi bali kuziachia mamlaka husika kushughulika na wahalifu wote.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso