Mratibu wa chanjo Mkoa Shinyanga,Timoth Sosoma amewaasa wananchi kujitokeza na kuondokana na Imani potofu katika zoezi la kupewa chanjo ya matone ya Polio awamu ya nne itakayotolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wapatao 521,025 hali itakayosaidia kuwalinda na ugonjwa huo.
Mratibu wa chanjo Mkoa Shinyanga ,Timoth Sosoma,wakati akieleza taarifa ya utekelezaji wa kampeni ya Chanjo ya Polio
NA HALIMA KHOYA, SHINYANGA.
Akizungumza leo,Novemba 29,2022 na waandishi wa habari, Mratibu wa chanjo Mkoa Shinyanga ,Timoth Sosoma,wakati akieleza taarifa ya utekelezaji wa kampeni awamu ya tatu na maandalizi ya kampeni ya awamu ya nne itakayofanyika Decemba Mosi hadi nne Mwaka huu.
Sosoma,ametumia nafasi hiyo kuwaasa wananchi kushirikiana vyema na wachanjaji wa chanjo hiyo ili kufikia malengo waliyojiwekea shanjari na kubainisha kuwa wataendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya faida za chanjo na athari za ugonjwa huo.
Aidha Sosoma,amebainisha kuwa zoezi la kampeni ya chanjo awamu ya nne litatolewa kwa watoto wote (wale waliopatiwa chanjo awamu ya pili na ya tatu),huku akieleza sehemu watakazo fikia kutoa huduma hiyo ni pamoja na Shuleni,Sokoni,na maeneo ya stendi ili kufanikiwa kuwapatia huduma hiyo kwa asilimia waliyojiwekea.
“awamu ya kwanza tulifanya vizuri tulikuwa na walengwa wapatao laki 349,000na waliochanjwa 445,681 sawa 128% na awamu ya tatu tulikuwa na walengwa laki 445,681 na waliopata chanjo ni laki 521 sawa sawa na asilimia 117%,na awamu hii ya nne chanjo hii itatolewa kwa watoto wapatao laki 521,021,huduma hii itatolewa kwenye wilaya 6(Kahama,,Kishapu,Msalala,Shinyanga mjini,Shinyanga vijijini,na Ushetu)”Amesema Sosoma.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu Mko Shinyanga,Faustine Mulyutu,Ameongeza kuwa wazazi na walezi wawapeleke watoto wao kupatiwa huduma hiyo sam,bamba na kubainisha kuwa hakuna maudhi yeyote yaliyojitokeza kwenye kampeni awamu ya pili na tatu.
Mulyutu amesema kumekuwa na mafaniko makubwa kwenye utolewaji wa chanjo hiyo wa watu wenye mahitaji maalum(Walemavu),ambapo wamekuwa wakifika katika mashule wanayoisomeshwa watoto hao.
Nao baadhi ya wazazi na walezi wanaishukuru serikali kuwaletea chanjo hiyo kwasababu wanatoa bure huku wakiahidi ya kuwa watawapeleka watoto wao kupatiwa huduma hiyo ili kuwa linda na kuwaepusha na ugonjwa huo.
No comments:
Post a Comment