VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHIMIZA MILA NA TAMADUNI ZA NCHI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Saturday, 19 November 2022

VIONGOZI WA DINI WATAKIWA KUHIMIZA MILA NA TAMADUNI ZA NCHI


Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa viongozi wa dini nchini kuhimiza Watanzania kuzingatia mila na tamaduni za kitanzania kwa lengo la kuimarisha misingi ya maadili.


Katika ufafanuzi wake, Rais Samia amesema malezi ya viongozi wa dini kwa vijana yamekuwa na mchango mkubwa katika kulinda Amani ya Taifa, kupunguza matukio ya uhalifu na kuimarisha huduma mbalimbali za kijamii ikiwamo afya na elimu.


Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumamosi Novemba 19, 2022 Jijini Dodoma wakati wa hotuba yake katika maadhimisho ya Jubilee ya Miaka 50 ya Utume na Huduma ya Kanisa la Waadventista Wasabato, Jimbo la Kati mwa Tanzania.


Ni sehemu ya zaidi ya miaka 100 ya kuanzishwa kanisa hilo linalotangaza habari njema za wokovu na kuimarisha Amani kwa watanzania kupitia neno la Mungu hapa duniani.


“Nimefurahishwa na kwaya mbili hapa, wameimba maudhui ya kizalendo na wamejengwa kizalendo. Kwa hiyo niwashukuru sana kwa malezi hayo, ni jambo jema sana kwani bila kuwa na vijana waadilifu, basi magereza yetu yangekuwa yamejaa,”amesema rais Samia mbele ya waumini wa kanisa hilo.


“Pia vyombo vya ulinzi na usalama vingekuwa na kazi ngumu sana ya kupishana pishana, huku Panya road, huku panya njia, huku nani sijui, hata majaji wetu wangekuwa na kazi kubwa sana, kwa hiyo niwasaidie sana kwa malezi na kukuza wazalendo, na huu ni wito kwa viongozi wetu wote.”


Jambo la tatu, alipongeza kanisa hilo katika ushiriki wa huduma za kijamii hususani sekta ya afya na elimu baada ya kujenga shule za awali, msingi na Sekondari ,Vyuo vya Ufundi Veta.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso