UPANDAJI WA PAMBA KWA KUCHIMBA MASHIMO NI CHANGAMOTO KWA WAKULIMA KISHAPU,MADIWANI WAIOMBA SERIKALI KUONGEZA MBEGU ZA PAMBA. - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Wednesday, 9 November 2022

UPANDAJI WA PAMBA KWA KUCHIMBA MASHIMO NI CHANGAMOTO KWA WAKULIMA KISHAPU,MADIWANI WAIOMBA SERIKALI KUONGEZA MBEGU ZA PAMBA.

MADIWANI wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu, wameiomba Serikali kuongeza usambazaji wa mbegu za Pamba kwa wakulima wilayani humo.

Waheshimiwa Madiwani Halmashauri ya Kishapu

NA HALIMA KHOYA, HUHESO DIGITAL - KISHAPU SHINYANGA.

Wamebainisha hayo leo Novemba 2, 2022 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wilayani Kishapu.


Wamesema kumekuwepo na changamoto kubwa ya uchache wa mbegu za Pamba kwa wakulima wilayani humo, ambao umesababishwa na wadudu kula mbegu hizo mashambani.


"Tangu tuanze kupanda pamba kumekua na changamoto ya uchache wa mbegu unaosababishwa na kuanzishwa kwa mbinu mpya ya kupanda pamba kwa kuchimba mashimo ambapo wadudu wanakuja kula mbegu hizo mashambani na kusababisha upungufu wa mbegu kwa wakulima,” amesema Michael Paulo diwani wa Shangihilu.


Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kishapu Emmanuel Johnson, ameahidi kulifanyia kazi suala hilo la usambazaji wa mbegu za kutosha kwa wakulima, hali ambayo itaongeza uzalishaji na halmashauri kupata mapato mengi ya kustosha.


Kwa upande wake Katibu Tawala wa wilaya ya Kishapu Shadrack Kengese, amewataka pia wananchi wilayani humo wajikite kwenye kilimo cha mazao ambayo yanastahimili ukame ili kuendana na mabadiliko ya tabia nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso