UKIKABILIWA NA NJAA NYUMBANI KWAKO UNAPELEKWA MAHAKAMANI - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Thursday, 10 November 2022

UKIKABILIWA NA NJAA NYUMBANI KWAKO UNAPELEKWA MAHAKAMANI

Mkuu wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Filbarto Sanga, amesema kuwa mkulima yeyote atakayebainika kukabiliwa na njaa atapelekwa mahakamani kutokana na kushindwa kufuata maagizo ya kuhifadhi chakula waliyopewa wakati wa msimu wa mavuno.
Mkuu wa wilaya ya Mlele mkoani Katavi, Filbarto Sanga

Akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo 2022/2023 uliofanyika Kata ya Usevya Halmashuri ya wilaya ya Mpimbwe, DC Sanga amesema tahadhari imetolewa mapema kabisa mwanzo wa msimu lakini baadhi ya wakulima wataingiwa na tamaa ya kuuza vyakula vyao vyote bila kuweka akiba ya kutosha.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mpimbwe Catherine Mashalah, ameshauri wakulima kupanda mbegu bora wakati wa mvua za kwanza ili mazao yapatikane kwa wingi.


Kwa upande wao wakulima wamekiri kupokea maelekezo hayo huku wakisema huwa wanauza mazao kwa sababu ya shida zinazowakumba ikiwemo magonjwa na kusomesha.

CHANZO:EATV

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso