Wananchi Mkoa Shinyanga wameaswa kutoa malezi bora kwa watoto wao(wakike na wakiume) pamoja na kuwapatia adhabu pindi anapochelewa kurudi nyumbani ili kusaidia kupunguza vitendo vya ukatili vinavyotokea katika jamii.
Katibu tawala wilaya ya Kishapu akitoa hotuba katika ufunguzi wa wiki ya sheria
NA HALIMA KHOYA,KISHAPU,SHINYANGA.
Hayo yamebainishwa Novemba 8,2022 katika uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya sheria duniani mbayo Mkoani Shinyanga yamezinduliwa katika kijiji cha Mwakipoya Wilaya Kishapu,huku kauli mbiu yake ni“Ukatili na udhalilishaji wa kijinsia ni kikwazo cha maendeleo”.
Akizungumza katika ufunguzi wa maadhimisho hayo,Katibu tawala Wilaya Kishapu,Shedrack kengese,Amesema katika jamii kumekuwa na wazazi wanaowalea watoto katika mazingira yasiyoridhisha pamoja na kutowapatia adhabu watoto wakichelewa kurudi nyumbani hali inayochochea vitendo vya ukatili.
Kengese,Amewataka wananchi wote kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria pale yanapotokea matukio ya ukatili ili kuwabainisha wanaohusika na matukio hayo hali itakayosaidia kupunguza wimbi la matukio hayo.
“Katika jamii kumekua na ukatili wa kijinsia ambayo sababu kubwa ni malezi na usimamizi hafifu wa wazazi kwa watoto wao,kuna kesi nilikamata mwenyewe tukamuuliza nani aliyekupatia mimba hii,akajibu ni Fulani,lakini alivyofika polisi anaulizwa nani ameekupatia ujauzito akakataa”Amesema Kengese.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya huduma Kisheria Mkoa Shinyanga,John Shija,Ameeleza dhima ya maadhimisho hayo ni kutatua changamoto zinazotokea katika jamii sambamba na ndoa za utotoni na ukatili wanaofanyiwa wanawake katika familia.
Mwenyekiti wa maadhimisho ya sheria mkoani Shinyanga Ndugu Shija John wakati akitoa elimu kwa jamii juu ya Sheria.
Kwa upande wake Afisa ustawi wa Jamii Mkoa Shinyanga,Lidya Kwesi,Ameitaka jamii kutoa ushirikiano kwa vyombo vya sheria ili kuondokana na adha ya matukio ya ukatili katika jamii sambamba na kubainisha kuwa ndani ya wiki hii watatoa elimu kwa jamii Mkoani humo.
Afisa Ustawi jamii Mkoa wa Shinyanga, akitoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment