Aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Mbunge wa Bukoba Vijijini mwaka 2005 hadi 2010 Nazir Karamagi, ametangazwa kuwa mshindi katika nafasi ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)mkoa wa Kagera.
Karamagi ametangazwa mshindi baada ya kupata kura 669 ambazo ni sawa na asilimia 58 ya kura zote zilizopigwa na kumshinda Costansia Buhiye aliyekuwa akitetea kiti hicho.
Buhiye amehudumu katika nafasi hiyo kwa muda wa miaka 15 na amepata kura 452 ambazo ni sawa na asilimia 32 ya kura zilizopigwa.
Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson ndiye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment