MIILI YA WAWILI WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE BUKOBA YAWASILI ARUSHA - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 8 November 2022

MIILI YA WAWILI WALIOFARIKI KWENYE AJALI YA NDEGE BUKOBA YAWASILI ARUSHA


Miili ya abiria wawili kati ya 19 waliofariki kwenye ajali ya ndege Precision Air iliyotakea Novemba 6, 2022 mkoani kagera imewasili mkoani Arusha kwa ajili ya maziko.



Miili hiyo ni ya Aneth Kaaya na Zaituni Mohamed ambao wamepokewa na Viongozi wa Serikali ya Mkoa wa Arusha kwa kushirikiana na familia zao katika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na hospitali ya Seliani na wanatarajiwa kuzikwa kesho.


Akizungumza katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Arusha Mount Meru baada ya kupokea miili hiyo, Mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Arusha ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Mhandisi Richard Ruyango amesema mwili wa Zaituni umehifadhiwa katika hospitali ya Seliani huku wa Aneth ukihifadhiwa Mount Meru.



"Tunaendelea kushukuru Mungu miili hiyo imefika salama ikiongozwa na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Kagera," amesema.


Naye Katibu wa CCM mkoa wa Kagera, Christopher Pallangyo amesema wamesafirisha miili mitatu ikiwa mmoja umeachwa wilaya Kondoa mkoani Dodoma kwa ajili ya mazishi.


"Miili miwili ni hii ambayo ni ya wadada zetu hivyo tunashukuru Mwenyezi Mungu tumesafiri salama kwani hatujapata tatizo lolote tukiwa njiani,"amesema Pallangyo.


Kaka wa marehemu Aneth, Frank Lameck amesema anaishukuru Serikali kwa kufanikisha mwili wa ndugu yao kufika nyumbani kwani alikuwa njiani kuelekea ukweni kutambulishwa lakini hakufanikiwa kutokana na umauti kumfika.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso