Mbunge wa jimbo la Kinondoni Abbas Tarimba, ameiomba serikali kutoa tamko rasmi kwamba dereva yeyote wa bodaboda atakayepita kwenye taa nyekundu, maeneo ambayo yamezuliwa na hata kubeba mishikaki akamatwe na kuchukuliwa sheria.
Mbunge wa jimbo la Kinondoni Abbas Tarimba
Kauli hiyo ameitoa hii leo Novemba Mosi, 2022, Bungeni jijini Dodoma, wakati wa kipindi cha maswali na majibu kwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi huku akisisitiza hatua hiyo ichukuliwe kufuatia uwepo wa changamoto kubwa kwa bodaboda kuzingatia sheria za barabarani.
"Serikali haioni sasa leo kutoa tamko kwamba bodaboda wote wanaopita kwenye taa nyekundu, no entries pamoja na kupakia mishikaki wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria?, amehoji Mbunge Tarimba
Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini amesema kuwa, ni kosa kubwa kwa bodaboda hata magari kupita kwenye taa nyekundu kwani ni kujiweka kwenye hatari zaidi.
"Askari wetu wa usalama barabarani huchukua hatua lakini mara nyingine imekuwa ni changamoto kwa upande wa viongozi wa kisiasa kuwatetea vijana hawa (Bodaboda), niombe tushirikiane sote, elimu tunatoa, sheria huchukuliwa lakini wote tuwe na utashi tuzungumze usalama barabarani hususani kwa vijana hawa wa bodaboda," amejibu Naibu Waziri Sagini
No comments:
Post a Comment