HESLB WAITWA KUJIELEZA IJUMAA KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI JE NI KUBURI AU - HUHESO DIGITAL BLOG

Breaking

Post Top Ad

Tuesday, 1 November 2022

HESLB WAITWA KUJIELEZA IJUMAA KUHUSU MIKOPO YA WANAFUNZI JE NI KUBURI AU


Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson ameitaka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB), kufika katika Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Ijumaa Novemba 4, 2022, ili kujieleza kwanini hawataki kusikiliza maelekezo ya Serikali.


Agizo hilo limefuatia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda na baadhi ya wabunge kulalamikia kuwa kamati aliyoiunda na (Profesa Mkenda), kuchunguza utoaji wa mikopo ya elimu ya juu imeshindwa kupata ushirikiano.


Dk Tulia ametoa uamuzi huo baada ya Bunge kujadili hoja ya uwepo wa wanafunzi wenye vigezo kukosa mikopo ya elimu ya juu, hoja iliyotolewa na Mbunge wa Biharamulo (CCM), Ezra Chiwelesa


“Naamini kwamba Waziri hawakusikilizi kwenye mambo mengine lakini kwenye hili watakusikiliza wao wataitwa katika Kamati yetu ya Huduma na Maendeleo ya Jamii…Siku ya Ijumaa saa 7.00 wajikute kwenye hiyo kamati,”amesema.


Tutatoa fursa tujue kama ni kiburi ama kitu kingine tofauti kwa ngazi hii. Kwa maana ya kuichunguza kama inatoa mikopo sawa sawa sio hoja wanazoitiwa ndani ya kamati, sasa hivi tunataka kuelewa kama Bunge kwa nini hiyo bodi haisikilizi hayo maelekezo,”amesema.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages

Huheso