WANANCHI katika Halmashauri ya Bukoba,wamehimizwa kutouza chakula kwa wingi hadi kufikia hatua ya kuuza akiba ya mbegu na hivyo kusababisha usumbufu wa kutafuta mbegu upya kwa ajili ya msimu unaofuata,na hivyo kuathiri upatikanaji wa chakula na ukosefu wa lishe bora na ya kutosha kwa watoto.
Na Mutayoba Arbogast,Huheso Digital - Bukoba
Hayo yameelezwa katika kikao cha Halmashauri ya Bukoba,kilichohusisha wakuu wa idara na shirika lisilo la liserikali la TADEP,ambalo pamoja na mambo mengine,linajihusisha pia na kutoa elimu ya lishe mkoani Kagera chini ya mradi wa Mtoto Kwanza na Proramu Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendekeo ya Awali ya Mtoto(PJT-MMMAM),kwa watoto miaka 0 hadi nane na kufanya utetezi kwa serikali ili mipango yake izingatie kuwekeza kwa maslahi ya watoto.
Kikao hicho kimeongozwa na Mganga mkuu wa wilaya,Dr Bandioti Gaviole,kwa niaba ya Mkurugenzi mtendaji wa wilaya kwa lengo la kuweka mpango kazi wa kuboresha na kuhuisha huduma za lishe katika bajeti ya mwaka 2022/2024.
Abimelack Richard,Afisa miradi wa shirika la TADEPA,amesema wanashughulikia maeneo matano yanayomhusu mtoto ambayo ni lishe,afya,ulinzi na usalama, uchangamshi na ujifunzaji wa awali.
Kwa upande wa lishe,Richard amesema shirika lake limekuwa likifuatilia kwa karibu upatikanaji wa chakula mkoani Kagera, kwamba mkoa unazalisha chakula cha kutosha,lakini tatizo ni pale baadhi ya wakulima wanapokuwa na tamaa ya fedha na hivyo kufikia hadi kuuza hata akiba ya mbegu ambayo wangeihifadhi kwa ajili ya msimu unaofuata.
"Hebu tujiulize,kwa nini wakati wa mavuno chakula kama mahindi na maharage hutoka vijijini kuja mjini,lakini wakati wa msimu wa kilimo,mazao hayo hayo kwa maana ya mbegu,hutoka mjini kwdnda vijijini?",alihoji Richard.
Akafafanua kwamba wakati wa msimu wa kilimo baadhi ya wakulima hujikuta hawana hata mbegu,na hivyo kulazimika kununua mbegu mjini kwdnye masoko,na wengine hata akiba ya hela waliyoipata walipouza mazao yao wzkati wa mavuno ilishakwisha,hivyo huangaika sana kupata mbegu,jambo linalosababisha baadhi ya familia kutokuwa na chakula cha kutosha na matokeo yake ni matatizo ya lishe kwa watoto wafogo na udumavu.
Amesema shirika lake limekuwa likihimiza juu ya umuhimu wa kutunza akiba ya chakula na mbegu,na njia sahihi za uhifadhi ili mazao hayo yasiharibike,na kuwa kuna umuhimu sana wa jambo hili kuwekwa kwenye mpango kazi ili liweze kuhimizwa na kutekelezwa kwa ngazi ya kaya.
Katika msimu wa kilimo 2017/2018 Mkoa ulijiwekea lengo la kulima na kutunza jumla ya hekta 679,393 za mazao mbalimbali ya chakula zilizotarajiwa kuzalisha jumla ya tani 2,592,695 za ndizi, tani 360,729 za nafaka, tani 170,053 za mikunde na tani 1,042,326 za mazao ya mizizi.
Hadi kufikia Mwezi Juni, 2018 Mkoa ulikuwa umelima na kutunza jumla ya hekta 673,974 za mazao mbalimbali ya chakula na kuzalisha jumla ya tani 2,379,901 za ndizi, tani 285,595 za nafaka, kati ya tani hizi, zao la mahindi limechangia uzalishaji wa tani 243,287, tani 122,406 za mikunde, aidha, zaidi ya tani 1,095,347 za mizizi zimezalishwa kati ya tani hizi, zao la mhogo limechangia uzalishaji wa tani 818,742.
Licha ya uzalishaji huu mubwa wa chakula,bado mkoa wa Kagera unaendelea kutajwa kuwa miongoni mwa mikoa kumi yenye udumavu kwa watoto
Mganga mkuu wa wilaya ya Bukoba,Dr Bandioti Gaviole amehimiza kuendelea kushirikiana kutekeleza Mpango Kazi Jumuishi wa pili wa Kitaifa wa Utekelezaji wa Afua za Lishe (National Multisectoral Nutrition Action Plan- NMNAP II 2020/21)ulio chini ya ofisi ya waziri mkuu,na kuhimiza kula mdau kuhakikisha suala la lishe bora nyjmbani na shuleni linapewa kipaumbele.
Kwa upande wa takwimu za kitaifa,serikali imefanikiwa kupunguza utapiamlo na ukondefu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano kutoka asilimia 4.5 (2015/16) hadi 3.5% (2018) ikiwa takribani watoto laki 6 huku akibainisha kuwa kazi bado iko kubwa kuelimisha jamii kuhusu Lishe bora.
No comments:
Post a Comment